Kasi ya mageuzi inahitajika Sudan Kusini: UM

21 Novemba 2013

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini Hilde Johnson amesema ili Sudan Kusini ipige hatua za kimaendeleoa hususani kuimarisha taasisi za kitaifa lazima isukume kasi ya mageuzi muhimu. Katika mahojiano maalum na mwandishi wa idhaa ya Kingereza ya radio ya Umoja wa Mataifa Don Bob, Bi Johnson amesema msingi wa demokrasi wa taifa hilo changa unategemea nia thabiti ya uongozi katika kuelekea njia ya mabadiliko

 

(Sauti Helde)

Hakuna shaka kwamba Sudan Kusini iko njia panda, jambo kubwa ni kuhakikisha mageuzi ya awali yanasukumwa katika utekelezaji wa masuala muhimu kama mageuzi ya usalama. Mgawanyo tunaoufanya mathalani kwa askari unaleta mabadliko lakini pia katika msingi wa demokrasia ya nchi katika maandalizi ya uchaguzi, kuna hatua kadhaa muhimu katika kuona uongozi huu wenye nia unasonga ambele katika mwelekeo sahihi

 

Akizungumzia changamoto zinazokabili ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS mwakilishi huyo wa katibu mkuu amesema ukosefu wa ndege za kijeshi ni upungufu ambao unasababisha vikosi vya ulinzi nchin humo kutonyumbulika sawia

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter