Mjadala wa Baraza Kuu wafunguliwa rasmi

24 Septemba 2013

Hatimaye mjadala Mkuu wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza Jumanne mjini New York, Marekani ukijumuisha viongozi wa nchi na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa huo. Wa Kwanza kuongea amekuwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe. Joshua Mmali ana taarifa kamili:

(TAARIFA YA JOSHUA)

JOHN ASHE Opener CLIP

Ni rais wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu, John William Ashe, akifungua mjadala wa leo.

Kabla ya kuanza rasmi kwa mjadala huo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon alitumia fursa hiyo kuelezea kazi za ofisi hiyo kuanzia masuala amani na usalama, ulinzi, maendeleo na uhifadhi wa haki za binadamu.

Amegusia mashambulizi huko Kenya, Somalia, Pakistani na matumaini yanayochipukia huko Afrika kufuatia uchaguzi nchini Mali na harakati za kuleta amani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bwana Ban akaelezea malengo ya maendeleo ya Milenia na vile ambavyo yameibua mafanikio makubwa katika kuyafikia licha ya changamoto zinazoendelea kuibuka katika baadhi ya nchi hususan utokomezaji umaskini. Amesema kuelekea ukomo wa malego ya milenia 2015, changamoto ni nyingi, mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na migogoro lakini akasema..

(Sauti ya Ban)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter