Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hebu tubadili jinsi tunavyoongoza kwa maslahi ya dunia yetu: Ban

Hebu tubadili jinsi tunavyoongoza kwa maslahi ya dunia yetu: Ban

Mjadala Mkuu wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza Jumanne mjini New York, Marekani ukijumuisha viongozi wa nchi na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa huo. Kabla ya kuanza rasmi kwa mjadala huo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon alitumia fursa hiyo kuelezea kazi za ofisi hiyo kuanzia masuala amani na usalama, ulinzi, maendeleo na uhifadhi wa haki za binadamu. Amegusia mashambulizi huko Kenya, Somalia, Pakistani na matumaini yanayochipukia huko Afrika kufuatia uchaguzi nchini Mali na harakati za kuleta amani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Bwana Ban akaelezea malengo ya maendeleo ya Milenia na vile ambavyo yameibua mafanikio makubwa katika kuyafikia licha ya changamoto zinazoendelea kuibuka katika baadhi ya nchi hususan utokomezaji umaskini. Amesema kuelekea ukomo wa malego ya milenia 2015, changamoto ni nyingi, mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na migogoro lakini akasema..

(Sauti ya Ban)