Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtembea bure si sawa na mkaa bure- Millard Ayo

Mtembea bure si sawa na mkaa bure- Millard Ayo

Pakua

Vijana ni nguvu kazi inayotegemewa katika kuboresha mustakabali wa dunia. Hata hivyo suala la  ajira limekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa kundi hilo katika maeneo mbalimbali duniani. Yaelezwa kuwa idadi kubwa ya vijana wanapomaliza shule huishia kufanya kazi zisizokuwa na tija katika maisha yao ilhali wanaweza kupata fursa an  ujuzi kwa njia tofauti na kuboresha maisha yao kama anavyoeleza Millard ayo kijana kutoka Tanzania ambaye anasema mwanzo wake ulikuwa na shubiri lakini bidii ndio imemwezesha kuchomoza na kujipatia umaarufu. Katika makala hii Patrick Newman alizungumza na Millard Ayo wakati alipotembelea Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjiin New York, Marekani na anaeleza kile alichofanya.

Photo Credit
Millard Ayo akivinjari New York, Marekani baada ya kutembelea Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/Patrick Newman)