ajira kwa vijana

Kufikia SDG’s ni ndoto iliyo mbali kwa mamilioni ya vijana wa MENA:UNICEF

Ripoti iliyotolewa leo na shirikala Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF inasema endapo serikali hazitotoa kipaumbele katika masuala ya amani na utulivu na kuwekeza katika mambo muhimu kwa ajili ya Watoto na vijana katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika , MENA, basi kanda hiyo itashindwa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 2030.

Ajira kwa vijana ni moja ya mtihani mkubwa unayoikabili dunia hivi sasa-ILO

Tatizo la ajira kwa vijana ni moja ya mtihani mkubwa unaoikabili dunia hivi sasa ambayo inahitaji suluhu ya pamoja kuitatua limesema shirika la kazi duniani ILO.

Wapiganaji wa zamani 126 wa Al-Shabaab walihitimu uanagenzi

Ukosefu wa amani na usalama nchini Somalia, umekuwa chanzo cha vifo na ukimbizi kwa wananchi iwe ndani  ya nchi yao au nje ya nchi huku kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kikiwa mara kwa mara kikijinasibu kushiriki kwenye mashambulizi hususan kwenye mji mkuu Mogadishu. 

Sauti -
2'52"

Ufundi stadi umesaidia vijana wengi Tanzania:VETA

Changamoto ya ajira ni kilio cha dunia nzima hususan kwa vijana ambao wengi hujikuta wakizurura mitaani au kuzungunga na vyetu vvyao wakisaka ajira ambazo zinazidi kuwa finyu kila uchao.

Sauti -
3'45"

Vijana watakiwa kutumia fursa za teknolojia zilizopo katika kujiajiri

Lengo namba  4 la ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya  maendeleo endelevu au SDGs, linahimiza serikali, asasi mbalimbali za kiraia na mashirika kutoa fursa ya  elimu bora na kukuza nafasi za masomo kwa vijana na jamii zote  ili kuweza kutokomeza umasikini .

Sauti -
3'53"

Kijana nchini Kenya abuni mashine ya kupiga chapa pande tatu au 3D

Lengo namba 9 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030 litaka ubunifu zaidi katika matumizi ya rasilimali ili kufanikisha malengo hayo yanayofikia ukomo mwaka 2030. Ubunifu hasa miongoni mwa vijana siyo tu unainua kipato bali pia unachochea maendeleo,

Sauti -
4'23"

Elimu ya ufundi, suluhisho la ukosefu wa ajira nchini Uganda.

Ukosefu wa ajira bado ni moja ya changamoto kubwa ulimwenguni kote hususan miongoni mwa vijana wanaohitimu masomo ambayo kwa kiasi kikubwa yamewaelekeza katika kazi za kuajiriwa.

Sauti -
3'40"

23 Novemba 2018

Leo hii katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Baraza la Biashara Afrika Mashariki lataka itifaki ya Kigali idhizie kote Afrika

-Ukata katika shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipastina , UNRWA watishia mustakabali wa watoto wa Kipalestina

Sauti -
11'47"

Jamii bado inashikilia mtazamo wa kazi fulani na jinsia fulani

Licha ya hatua zilizopigwa katika usawa wa kijinsia hususan sekta ya ajira lakini bado kuna pengo kubwa katika usawa wa kijnsia katika kazi zinazohitaji stadi za kiwango cha juu.

Sauti -
3'33"

ILO yasaidia stadi za kazi kwa magenge ya zamani ya uhalifu Madagasacar

Shirika la kazi duniani, ILO nchini Madagascar linaendesha mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana wasio na ajira hususan wale waliokuwa wafuasi wa magenge  ya uhalifu ili hatimaye waweze kuajiriwa au kujiajiri.