Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masahibu ya wasaka hifadhi Ulaya na matumaini yao yawekwa bayana

Masahibu ya wasaka hifadhi Ulaya na matumaini yao yawekwa bayana

Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi baada ya kufurushwa makwao ni zaidi ya watu milioni 60, na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Wakimbizi, UNHCR. Shirika hilo linasema mwaka 2010 idadi ya watu waliokimbia makwao kila siku ni Elfu Kumi na Moja, idadi ambayo imefikia Elfu 42 mwaka jana. Wengi wa wakimbizi na wahamiaji hao wanatoka nchini Syria, ambako mapigano ya miaka mitano, yamelazimu watu wengi kukimbilia bara Ulaya.

Miongoni mwao ni Humana, mama wa kipalestina aliyekuwa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Yarmourk nchini Syria.

Masaibu mengi aliyokumbana nayo njiani katika safari yake na kufahamu masaibu hayo sawa na matumaini yake maishani, ungana na Abdullahi Boru kwenye makala hii.