Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Wananchi wanaelewa kuhusu mabadiliko ya tabianchi baada ya kuiona hali halisi
Mafuriko, mvua za kupindukia, ukame na kuyeyuka kwa barafu ni ishara kubwa ya mabadiliko ya tabianchi lakini ni hadi wakazi wa ulimwengu wayashuhudie ndipo wanaamini, hivyo ndivyo anavyoeleza Kaimu Afisa Mazingira wa wilaya ya Pangani katika mahojiano na Saa Zumo wa Redio washirika Pangani FM, kuhusu hatua na harakati zinazofanywa na mamlaka ya wilaya ya Pangani katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
27 APRILI 2020
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Watoto wengi wakosa chanjo hata kabla ya kuzunga kwa janga la virusi vya Corona au COVID-19 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likitaka hatua madhubuti zichukuliwe sasa kuhakikia watoto wanapata chanjo zote
-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo limeanza kusambaza mashine za hewa ya Oxygen katika vituo sita vya afya vinavyohudumia wagonjwa wa COVID-19