Baraza la Usalama lakutana kujadili mashambulizi ya Marekani huko Syria na Iraq
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu alasiri limekuwa na kikao cha dharura kufuatia ombi la Urusi, wakati huu ambao vita huko Gaza inaendelea kuchochea mivutano huko Mashariki ya Kati, hasa uwezekano wa kuathiri vibaya amani na usalama kwenye ukanda huo. Mkuu wa Idara ya UN ya Masuala ya Kisiasa, ameliomba Baraza lizuie kushamiri zaidi kwa uhasama na mivutano kwenye ukanda mzima