TANBAT 6 wafanya usafi na kutoa msaada wa vifaa tiba CAR
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutokaTanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA wametoa misaada mbalimbali kwa jamii wanazolinda kama moja ya sehemu ya kuimarisha utangamano na maelewano kati yao na jamii wanayoilinda. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Kapten Mwijage Inyoma.