Mwambata jeshi wa Tanzania nchini CAR asifu utimamu wa wanajeshi wa Tanzania
Mwambata jeshi wa Tanzania anayehudumu kazi yake Jamhuri ya Afrika ya kati Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi amefanya ziara ya kutembelea kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA ili kujitambilisha tangu kikosi hicho kianze shughuli ya ulinzi wa amani kikipokea majukumu kutoka kwa kikosi cha TANBAT5 mwishoni mwa mwaka jana.