Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwambata jeshi wa Tanzania nchini CAR asifu utimamu wa wanajeshi wa Tanzania

Mwambata wa jeshi Brigedia Generali Absolomon Lyanga Shausi akisalimiana na Afisa wa Polisi wa NEPAL iliyopo chini ya MINUSCA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kujitambulisha kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanahudumu chini ya MINUSCA nchini CAR.
TANBAT 6

Amani na Usalama

Mwambata jeshi wa Tanzania anayehudumu kazi yake Jamhuri ya Afrika ya kati Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi amefanya ziara ya kutembelea kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA ili kujitambilisha tangu kikosi hicho kianze shughuli ya ulinzi wa amani kikipokea majukumu kutoka kwa kikosi cha TANBAT5 mwishoni mwa mwaka jana.

Ziara hiyo ilianza Kwa kupokelewa kwa Mkuu huyo na kamanda kikosi cha 6 cha walinda amani kutoka Tanzania, Luteni kanali Amani Stephene Mshana katika uwanja wa ndege wa BERIBERATI, kisha paredi ya heshima.

Maafisa walianza Kwa kumkaribisha mwambata jeshi Brigedia Generali Absorom Lyanga Shausi Kwa kuimba nyimbo za morali. Kisha Mkuu huyo aliongea na maafisa na askari huku akiwasisitiza kuendeleza umoja.

“Nimeshuhudia walinda amani walivyojipanga, nivigumu kutofautisha kwamba huyu ni watanzania na huyu ni wa Nepal, wanatekeleza majukumu yao kwa ushirikiano kama vile wamejengwa kama jeshi moja.”

Brigedia Shausi amesifu pia utimamu wa jeshi la Tanzania “Umahiri ambao umeoneshwa na jeshi la Tanzania unaonesha kiwango cha nidhani ambacho wanayo.”

Mkuu wa kikosi Cha TANBAT6 luteni kanali Amini Stephen Mshana  akimsindikiza mwambata jeshi Brigedia Generali Absoromon Lyanga Shausi uwanja wa ndege wa Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï nchini CAR.

Akitoa shukurani zake na za kikosi cha TANBAT6 Luteni kanali Amini Stephen MShana alisema Kuwa amempokea Kwa furaha kubwa mwambata jeshi aliyekuja kujitambulisha lakini pia kuona utimamu na utayari wa kikosi hicho kilichopo chini ya MINUSCA na kuahidi kudumisha aliyelekezwa katika utendaji wa ulinzi wa amani nchini Afrika ya kati.

Taarifa hii imeandaliwa na kapteni Mwijage Inyoma aliyeko nchini Afrika ya Kati.