Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mwandishi wa habari akitangaza katika Radio Miraya nchini Sudan Kusini.
UNMISS/Isaac Billy

Radio na nafasi yake ya ujenzi wa amani

Hii leo ni siku ya redio duniani ambapo Umoja wa Mataifa unamulika nafasi ya chombo hicho kilichobuniwa takribani karne moja iliyopita katika kukuza na kujenga amani  wakati huu ambapo pia ni miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Sauti
1'44"
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akikutana na Nour mtoto aliyepoteza wazazi wake wote kwenye tetemeko la ardhi Aleppo, Syria
WHO

Dkt. Tedros azindua ombi la kibinadamu kusaidia waathirika wa matetemeko Syria na Uturuki:WHO 

Katika ziara yake nchini Syria, mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo Jumapili amezindua ombi la kibinadamu la kukusanya dola milioni 43 kusaidia juhudi za kukabiliana na athari Syria na Uturuki baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyozikumba nchi hizo mbili wiki moja iliyopita na kusababisha vifo, watu kutawanywa na kujeruhi makumi ya maelfu ya watu. 

Familia moja kutoka eneo la Rumaila katika wilaya ya Jableh, kaskazini magharibi mwa Syria wakisimama karibu na nyumba yao iliyoharibiwa.
© UNICEF/Hasan Belal

Pedersen ataka siasa ziwekwe kando na kuungana kuwasaidia Wasyria walioathirika na tetemeko

Baada ya kuwasili Damascus, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, Geir Pedersen, ametoa tena salamu zake za rambirambi kwa watu wa Syria kwa hasara kubwa iliyotokana na tetemeko la ardhi na kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unafanya kila linalowezekana ili kutoa msaada unaohitajika kwa watu hao walioathirika.