Haki za binadamu ziwe muongozo wa vita dhidi ya COVID-19:UN
Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba haki za binadamu zinapaswa kuwa muongozo katika hatua zinazochukuliwa kupambana na janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19.
Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba haki za binadamu zinapaswa kuwa muongozo katika hatua zinazochukuliwa kupambana na janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19.
Wiki ya chanjo duniani ikianza kesho, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limeonya kuwa kufunga huduma za chanjo wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, kunaweza kusababisha kuibuka kwa janga la magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, limechukua hatua kuhakikisha kuwa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, vifaa vya matibabu pamoja na wafanyakazi wanaweza kufika popote pale wanapohitajika kwa wakati.
Janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID -19 limedhihirisha umuhimu wa teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA au ICT kwa wasichana na dunia nzima umesema Umoja wa Mataifa.
Kushuka kwa kiwango cha gesi chafuzi kunakohusiana na mlipuko wa janga la virusi vya corona au COVID-19 ni Habari njema za muda mfupi kwa mujibu wa mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC imeendelea na kampeni ya chanjo dhidi ya milipuko ya ugonjwa wa Surua kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo wakati huu ambapo taifa hilo linakabiliana pia na mlipuko wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake nchini Bangadesh wanachukua kila tahadhari ili kuhakikisha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kwenye moja ya makazi makubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Cox's Bazaar wanalindwa dhidi ya mlipuko wa Corona au COVID-19.
Janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19 limefanya macho yote ya Dunia kuelekezwa kwenye mtihani huu mkubwa zaidi ambao ulimwengu umekumbana nao tangu Vita vya Pili vya Dunia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Nchini Kenya ambako tayari mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, umesababisha vifo huku wagonjwa wapya wakiendelea kuripotiwa, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaunga mkono harakati za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo ambavyo hadi sasa havina tiba wala chanjo.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limetoa mwongozo mpya wa kuweza kusaidia kubaini mapema ukosefu wa madini ya chuma mwili sambamba na uwepo wa madini mengi ya aina hiyo kupita kiasi mwilini.