Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasaidia DRC kuendeleza chanjo dhidi ya Surua

Mtoto akifarijiwa na muhudumu wa afya wakati akisubiri kupatiwa chanjo ya surua kwenye kituo cha afya cha wilaya ya Nsele Congo DRC
© UNICEF Patrick Brown
Mtoto akifarijiwa na muhudumu wa afya wakati akisubiri kupatiwa chanjo ya surua kwenye kituo cha afya cha wilaya ya Nsele Congo DRC

UNICEF yasaidia DRC kuendeleza chanjo dhidi ya Surua

Afya

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC imeendelea na kampeni ya chanjo dhidi ya milipuko ya ugonjwa wa Surua kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo wakati huu ambapo taifa hilo linakabiliana pia na mlipuko wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19.

Kampeni hiyo dhidi ya Surua iliyoanza Jumanne wiki hii ya tarehe 21 mwezi Aprili inafanyika kwa usaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa kuzingatia kuwa tangu tarehe 1 mwezi Januari mwaka huu, wagonjwa 3,167 wa Surua wameripotiwa jimboni Kivu Kaskazini na wengi wao ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

UNICEF inasema kuwa hiyo inalenga watoto 150,491 wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi miaka 5 katika kanda 7 za kiafya za jimbo la Kivu Kaskazini zilizoathirika zaidi.

Kanda hizo ni Beni, Mabalako, Manguredjipa, Bambo, Birambizo, Mweso na Nyragongo.

Shirika hilo linasema kuwa kanuni za utoaji wa chanjo zimefanyiwa marekebisho ili kuepusha maambukizi ya COVID-19 ambapo walezi au wazazi na watoto pekee ndio wataruhusiwa kuingia vituo vya afya wakati katika vikundi vidogo vidogo.

Mathalani kila mtu anatakiwa kuwa mita moja kutoka mwenzake huku UNICEF ikihakikisha kuwa vifaa kando ya chanjo vinakuwepo ikiwemo vile vya kujikinga kama vile glovu na barakoa kwa ajili ya wahudumu wa afya.

Hata hivyo watoto na walezi na wazazi nao pia watatakiwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, huduma ambazo zitapatikana kwenye vituo vya chanjo.

Akizungumzia kampeni hiyo, mkuu wa ofisi ya  UNICEF, kwenye mji wa Goma huko Kivu Kaskazini, Frederic Emirian amesema kuwa, “chanjo inasalia kuwa hatua muhimu ya kuokoa maisha. Ni muhimu sana kuendeleza chanjo huku tukihakikisha kuwa hatua za kujikinga dhidi ya COVID-19 zinazingatiwa na wahudumu wa afya wanapatiwa mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao.”

Kati yam waka 2019 na 2020, gonjwa la Surua lilishika kasi huko DRC ambapo wagonjwa zaidi ya 332,000 waliripotiwa na kati yao hao 6,200 walifariki dunia kati yao hao asilimia 85 wakiwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

TAGS: DRC, Kivu Kaskazini, UNICEF, Goma