Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake nchini Bangadesh wanachukua kila tahadhari ili kuhakikisha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kwenye moja ya makazi makubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Cox's Bazaar wanalindwa dhidi ya mlipuko wa Corona au COVID-19.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake nchini Bangadesh wanachukua kila tahadhari ili kuhakikisha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kwenye moja ya makazi makubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Cox's Bazaar wanalindwa dhidi ya mlipuko wa Corona au COVID-19.
Kwenye makazi ya wakimbizi wa Rohngya Cox’s Bazaar nchini Bangladesh pilika ni nyingi lakini pia maandalizi ya kujikinga na janga la mlipuko wa corona.
Ingawa hakuna mgonjwa hata mmoja hadi sasa kwenye makazi haya yenye wakimbizi karibu laki 8, UNHCR inakimbizana na wakati ili kuhakikisha kuna huduma za afya na mahitaji mengine ya msingi ya kujikinga na janga hilo endapo litazuka.
Miundombinu na huduma zilizopo kwenye makazi haya zimezidiwa uwezo.Sasa UNHCR imelivalia njuga suala hilo ukizingatia kwamba virusi vya Corona vinasambaa kila kona ya dunia na hofu yao kubwa ni kuingia katika makazi haya kwani linasema si suala la endapo litawasili bali ni lini litawasili. Sandra Harlass ni afisa wa afya wa UNHCR anasema wanajiandaa kwa kila njia
Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.
“Katika makambi ya wakimbizi kwa mfano tumewapa mafunzo maafisa wa afya wa kijamii 1,2000 ili kusambaza ujumbe wa usafi, wa kueleza COVID-19 ni nini , dalili zake, jinsi gani ya kujikinga kama familia na vipi kutochangamana kunaweza kusaidia kujilinda.”
Mbali ya mafunzo pia UNHCR inasambaza vifaa muhimu vinavyohitajika kama anavyosema Santanu Sarma afisa msaidizi wa UNHCR
“UNHCR katika kambi ya Cox’s Bazaar imechukua tahadhari zote na kuongeza mara mbili ugawaji wa sabuni, pamoja na vifaa vya wanawake kujisafi kambini. Na pia kuna taratibu zilizowekwa kuhakikisha watu hawachangamani.”
Kwa mujibu wa UNHCR pamoja na jitihada zote hizi msaada wa kimataifa unahitajika hasa kushughulikia masuala kama elimu, usajili, na kuwalinda wakimbizi wasiojiweza kama watoto, wanawake na watu wenye mahitaji maalum.
Pia shirika hilo linasaidiana na serikali ya Bangladesh katika maandalizi ya kukabiliana na COVID-19 endapo itazuka kambini hapo wakati huu wakimbizi wakijiandaa na msimu wa mvua kubwa za monsoon.
TAGS:COVID-19, coronavirus, Bangladesh, Cox'sBazaar, Rohingya, UNHCR