Taarifa ya takwimu za sasa kuhusu kipindupindu Zimbabwe
UM umeripoti takwimu za wagonjwa waliopatwa na kipindupindu katika Zimbabwe leo hii ni 23,712 na jumla ya vifo kwa sasa kutokana na maradhi ni 1,174.
UM umeripoti takwimu za wagonjwa waliopatwa na kipindupindu katika Zimbabwe leo hii ni 23,712 na jumla ya vifo kwa sasa kutokana na maradhi ni 1,174.
Vikosi Mseto vya UM/UA vya Kulinda Amani Darfur (UNAMID) vimearifu askari 45 wa Kombania ya Usafiri Wastani ya Jeshi la Ethiopia waliwasili karibuni katika Darfur Magharibi. Kombania hii ya majeshi ya Ethiopia itatumiwa kugawa shehena za mizigo na vifaa baina ya kambi za walinzi wa amani wa UNAMID, ikijumlisha ugawaji wa maji na matangi ya nishati, na vile vile kuwapatia wanajeshi usafiri.
Wataalamu wanne wa UM juu ya haki za binadamu leo wametoa mwito maalumu wenye kuhimiza Serikali ya Zimbabwe pamoja na jumuiya ya kimataifa kuongeza mchango wao kwenye misaada ya kiutu kuwahudumia bora umma dhaifu na kukomesha janga liliotanda nchini la maradhi ya kipindupindu.
Ijumatatu KM alitoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, iliyopongeza ripoti za kuwachiwa kutoka kifungo cha nyumbani Raisi wa Mauritania, Sidi Ould Cheikh Abdallahi, ambaye serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu.
Kwenye mkutano mkuu wa siku tatu, wa kiwango cha mawaziri, uliofanyika kwenye mji wa Sirte, Libya wiki iliopita, kujadilia miradi ya kutunza maji kwa kilimo na kuzalishia nishati katika Afrika, kulikubaliwa rai ya kuchangisha mabilioni ya dola kukidhia mipangop hiyo ya maendeleo.
Baraza la Usalama Ijumatatu linazingatia ripoti juu ya mapendekezo ya UM ya kuongeza muda wa operesheni za shirika la ulinzi amani katika JKK, MONUC, kwa mwaka mmoja zaidi mpaka tarehe 31 Disemba 2009.
Baraza la Usalama Ijumatatu limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za MONUC, yaani lile Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK, kwa mwaka mmoja zaidi.Vile vile Baraza lilipiga kura ya kuendeleza vikwazo dhidi ya JKK mpaka mwisho wa Novemba 2009.~
Wiki hii, kwenye mji wa Sirte, Libya kulifanyika Mkutano Mkuu wa siku tatu, wa kiwango cha mawaziri, kwa madhumuni ya kuzingatia “Utunzaji wa Maji kwa Kilimo na Uzalishaji Nishati katika Afrika”. Ripoti yetu inaelezea, kwa kifupi, lengo hakika la mkutano, ikijumuisha na fafanuzi za Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya juu ya mijadala ya kikao.~

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetoa mwito wa kutaka lifadhiliwe msaada wa dola milioni 92 ili kufarajia kihali Wasomali 250,000 waliosibika na matatizo ya makazi kwenye kambi kongwe za wahamiaji za Dadaab, ziliopo Kenya mashariki, karibu na mipaka na Usomali.