Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Msanii S. Heitzeg aifadhilia UM hidaya ya utunzi wa 'Wimbo usio Mipaka'

Mapema Ijumatano asubuhi ya tarehe 19 Agosti 2008 walikusanyika Makao Makuu ya UM aila ya UM - ikijumuisha KM BAN Ki-moon - kwenye taadhima maalumu za kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu ofisi za UM ziliporipuliwa kwa bomu liliopakiwa lori iliogeshwa karibu na majengo ya Hoteli ya Kanali, yalipokuwa ofisi za UM mjini Baghdad. Shambulio lilitukia tareheb 19 Agosti 2003.

Hapa na pale

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM ju ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumaa alizuru Ossetia Kusini kusailia mahitaji ya umma uliodhurika na mzozo uliofumka huko mnamo 07 Agosti 2008. Guterres ni ofisa mkuu wa kwanza wa UM kuzuru eneo hili tangu machafuko kuzuka. Alisema UNHCR itaendelea kupeleka misaada ya kiutu kwenye eneo kuhudumia mahittaji ya umma mwaathiriwa, na bila ya kufungamana misaada na itikadi za kisiasa. Alisisitiza misaada ya kiutu haitolewi kwa kubagua, bali hufadhiliwa kila mtu muhitaji anayeathiriwa na maafa kwa kulingana na dharura iliopo kwenye maeneo yao. Vile vile Guterres alitilia mkazo kwamba wahamiaji wote waliong’olewa makaazi kwa sababu ya mapigano wana haki, kwa sheria ya kimataifa, kurejea makwao pale wanapohisi hali inawaruhusu. Kamishna Mkuu Guterres Ijumaa alikamilisha ziara ya siku nne kieneo kufanya tathmini, ya binafsi, kuhusu hali, kwa ujumla, katika Georgia na Shirikisho la Urusi ambapo uhasama ulishtadi katika siku za nyuma. ~

Majadiliano ya kina yameanza Ghana kusailia mkataba wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Wawakilishi 1,600 kutoka nchi wanachama 160 wamekusanyika hivi sasa kwenye mji wa Accra, Ghana kuhudhuria kikao cha wiki moja (21-27 Agosti 2008)kujadilia nidhamu za kuchukuliwa kipamoja kudhibiti bora tatizo la hewa chafu inayomwagwa angani, tatizo ambalo limethibitika kuwa ndio lenye kuharibu mazingira na kutifua mabadiliko ya kigeugeu ya hali ya hewa kimataifa. Mkutano umeandaliwa na Taasisi ya UM juu ya Mfumo wa Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC).