UNAMIL imeripoti tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zimepungua Liberia
Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Liberia (UNMIL) limewasilisha ripoti mpya kuhusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia nchini, yanayoambatana na watumishi wa UM. Kwa mujibu wa ripoti, idadi ya shutuma za makosa hayo dhidi ya wafanyakazi wa UNMIL imeteremka katika 2008.