Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM ju ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumaa alizuru Ossetia Kusini kusailia mahitaji ya umma uliodhurika na mzozo uliofumka huko mnamo 07 Agosti 2008. Guterres ni ofisa mkuu wa kwanza wa UM kuzuru eneo hili tangu machafuko kuzuka. Alisema UNHCR itaendelea kupeleka misaada ya kiutu kwenye eneo kuhudumia mahittaji ya umma mwaathiriwa, na bila ya kufungamana misaada na itikadi za kisiasa. Alisisitiza misaada ya kiutu haitolewi kwa kubagua, bali hufadhiliwa kila mtu muhitaji anayeathiriwa na maafa kwa kulingana na dharura iliopo kwenye maeneo yao. Vile vile Guterres alitilia mkazo kwamba wahamiaji wote waliong’olewa makaazi kwa sababu ya mapigano wana haki, kwa sheria ya kimataifa, kurejea makwao pale wanapohisi hali inawaruhusu. Kamishna Mkuu Guterres Ijumaa alikamilisha ziara ya siku nne kieneo kufanya tathmini, ya binafsi, kuhusu hali, kwa ujumla, katika Georgia na Shirikisho la Urusi ambapo uhasama ulishtadi katika siku za nyuma. ~