Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Upungufu wa fedha kuilazimisha WFP kupunguza shughuli Sudan

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba litalazimika kupunguza huduma zake za anga, zinazotumiwa kugawa misaada ya chakula kwa umma muhitaji katika eneo la mgogoro la Darfur, na kwenye sehemu nyengine zilizotawanyika masafa kadha wa kadha nchini Sudan.

Wajumbe wa Baraza la Usalama wamewasili Cote d'Ivoire kukamilisha ziara ya Afrika

Tume ya wajumbe wa Baraza la Usalama wanaozuru Afrika imewasili Cote d\'Ivoire Ijumapili, wakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ziara yao baada ya kutembelea mataifa ya Djibouti, Sudan, Chad na JKK. Ijumatatu wajumbe wa tume ya Baraza la Usalama wamefanyisha mazungumzo mjini Abidjan na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Cote d\'Ivoire, Chuo Young-Jin na maofisa wengine wa ngazi za juu wa UM wanaohusika na huduma za amani nchini humo.

Mwanahabari mzalendo kauawa na majambazi Usomali

Mark Bowden, Mshauri Mkaazi wa UM juu ya Misaada ya Kiutu kwa Usomali ameripoti kuwa ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji ya Nasteh Dahir Farah, mwandishi habari mzalendo, aliyeajiriwa na shirika la habari la Uingereza, BBC pamoja na shirika la Associated Press, mauaji ambayo yalitukia tarehe 07 Juni katika mji wa Kismayo, ambapo iliripotiwa alipigwa risasi na majambazi wasiojulikana.

Eneo zima la Darfur lizingatiwe mazingira ya uhalifu, imeonya ICC

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) alipohutubia kikao cha hadhara cha Baraza la Usalama Alkhamisi, kuhusu matokeo ya uchunguzi juu ya hali katika Darfur, alisema ana ushahidi wa kutosha uliothibitisha vitendo haramu vilivyokiuka kanuni za kimataifa vinafanyika kwenye eneo hilo la Sudan.

Mkutano wa Kudhibiti Mzozo wa Chakula Duniani umeahidi misaada maridhawa kwa mafukara muhitaji wa kimataifa

Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani uliofanyika mjini Roma, Utaliana ulikhitimishwa Alkhamisi baada ya siku tatu ya majadiliano makali miongoni mwa Mataifa Wanachama. Ripoti ya mwisho iliopitishwa iliahidi jamii ya kimataifa itajumuika kipamoja "kukomesha njaa pote ulimwenguni na kudhaminia kupata chakula ule umma muhitaji bilioni moja, hivi sasa na katika miaka ijayo." ~

Mashambulio ya raia Kivu Kaskazini kulaaniwa na UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limelaani mashambulio yaliotukia kwenye kambi ya muda iliopo eneo la mashariki katika JKK ambapo iliripotiwa watu karibu tisa waliuawa, wakiwemo watoto wadogo wawili, na korja ya watu wengine kujeruhiwa. UNHCR pamoja na mashirika yanayohudunmia misaada ya kiutu yameamua hivi sasa kusitisha operesheni zao na kuhamisha wafanyakazi, kwa muda, kutoka eneo la Kivu Kaskazini, kilomita 70 kaskazini ya mji wa Goma.~