Skip to main content

Tume ya Baraza la Usalama imezuru Darfur, na imekutana na viongozi wa Sudan

Tume ya Baraza la Usalama imezuru Darfur, na imekutana na viongozi wa Sudan

Wajumbe wa tume maalumu ya Baraza la Usalama Alkhamisi walizuru ElFasher mji mkuu wa Darfur Kaskazini na kukutana kwa mashauriano na wanajeshi wa vikosi mseto vya UM na UA kwa Darfur (UNAMID) pamoja na Mkuu wa UNAMID, Rodolphe Adada baada ya kuzuru kambi za wahamiaji wa ndani wa IDPs ya Zam Zam.