Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa kimataifa wakutana Makao Makuu kuzingatia hatua za kupiga vita UKIMWI na TB

Viongozi wa kimataifa wakutana Makao Makuu kuzingatia hatua za kupiga vita UKIMWI na TB

Baraza Kuu la UM Ijumanne litaanzisha majadiliano muhimu ya hadhi ya juu, yatakayochukua siku mbili (10 - 11 Julai), kufanya mapitio kuhusu utekelezaji wa zile Ahadi za 2001 pamoja na Mapendekezo ya Mwito wa 2006 katika Kupiga Vita UKIMWI Duniani.

Vile vile Tume inayohusika na UKIMWI na Juhudi za Utawala Afrika imewasilisha ripoti maalumu ya kuzingatiwa kwenye majadiliano, yenye muktadha usemao "Ulinzi wa Maisha ya Wakati Ujao".

Halkadhalika, Ijumatatu, siku moja kabla ya mkutano wa mapitio kuanza mijadala yake, kumeandaliwa semina maalumu katika Makao Makuu iliowakilisha viongozi wa serikali, maofisa wanaohusika na huduma za afya na biashara, wakuu wa mashirika ya UM pamoja na wanaharakati wa kimataifa ambao walibadilishana mawazo juu ya namna ya kukabiliana na maradhi ya kifua kikuu katika Afrika, magonjwa ambayo ndio chanzo kinachochea vifo kwa idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU.