Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mjumbe wa KM anasema mwafaka wa Uganda na waasi unaashiria matumaini mema

Raisi mstaafu wa Msumbiji, Joaqim Chissano, ambaye ni Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Tatizo la waasi wa LRA Uganda alianza ziara ya upatanishi Uganda Ijumaa iliopita. Baada ya hapo Chissano alielekea Juba, Sudan Kusini kuendelea na mazuungumzo ya upatanishi baina ya Serikali ya Uganda na waasi wa LRA. Msuluhishi Dktr. Riek Machar Dhurgon Teny, aliye naibu-raisi wa Serikali ya Sudan Kusini naye pia amejumuika kwenye majadiliano hayo.~~

Eritrea imezuia Walinzi wa usalama wa UM kuingia Ethiopia

Wenye madaraka Eritrea wamekataa kuwaruhusu watumishi wa Shirika la UM la Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE) kwenda Ethiopia, hali ambayo iliwalazimisha kurejea mjini Asmara kusubiri ushauri kutoka UM juu ya hatua za kuchukuliwa nawo baada ya mvutano huu. Tukio la kuwazuia walinzi wa amani kutovuka mpaka limejiri licha ya kuwa Ijumaa iliopita Baraza la Usalama lilishtumu vikali "ukosefu wa ushirikiano" kutoka Serikali ya Eritrea, ambaye ililaumiwa kujitenga na majukumu yake ya kusaidia vikosi vya UNMEE kudhibiti bora usalama kwenye eneo la mgogoro mipakani.

'Wadudu si kero bali hurutubisha lishe', yanasihi FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kwamba aina 1,400 za wadudu wanaokutikana kwenye misitu ya dunia huliwa na wanadamu. FAO imetayarisha pamoja na Chuo Kikuu cha Chiang Mai,Thailand wiki hii warsha wa siku tatu ambapo wataalamu wa kimataifa wanazingatia uwezekano wa kuanzisha biashara ya wadudu, kwa chakula, katika maeneo ya Asia na ukanda wa Pasifiki, ikiwa miongoni mwa juhudi za kupunguza tatizo la njaa duniani. Wadudu wanaoliwa na wanadamu wamegunduliwa kurutubisha pakubwa lishe. ~

Mjumbe wa vijana asailia kikao cha CSD juu ya maendeleo

Neema Buhile, ni mwakilishi wa Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola kutokea Tanzania ambaye hivi majuzi alikuwepo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UM) kuhudhuria kikao cha mwaka cha Kamisheni juu ya Maendeleo ya Jamii (CSD). Muktadha wa mkutano huo wa mwaka ulilenga zaidi yale masuala yanayofungamana na ajira, ulemavu, hali ya kuzeeka na pia vijana. Redio ya UM ilipata fursa ya kuzungumza na Neema ambaye alitupatia maoni yake kuhusu ushirikiano unaofaa kuendelezwa na wajumbe wa kimataifa ili kuyatekeleza mapendekezo ya vikao vya kimataifa, kama kikao cha mwaka CSD, kwa mafanikio. ~~Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Fafanuzi za Mjumbe wa Tanzania juu ya kikao cha Kamisheni ya CSD

Naibu KM Asha-Rose Migiro alifungua rasmi kikao cha 46 Kamisheni ya CSD wiki iliopita ambapo alitilia mkazo kwenye hotuba yake juu ya “jukumu muhimu la ajira na kazi stahifu katika kukuza maendeleo”, hususan kwenye nchi zinazoendelea. Ernest Ndimbo, Mkurugenzi wa Ajira kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Watoto Tanzania alikuwa miongoni mwa wawakilishi waliohudhuria mkutano wa Kamisheni ya CSD. Ndimbo alifanya mahojiano maalumu na Redio ya UM ambapo alichukua fursa hiyo kutupatia fafanuzi zake kuhusu kikao cha mwaka huu cha Kamisheni ya CSD.~