Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimu wa sayansi ya polisi kufunza vikosi vya ulinzi wa amani kwa Darfur

Walimu wa sayansi ya polisi kufunza vikosi vya ulinzi wa amani kwa Darfur

Tangu Ijumatatu, walimu wa kimataifa wa mafunzo ya polisi, wenye vyeo vya juu, wameanzisha mafunzo kwa maelfu ya polisi wa UM juu ya taratibu za kudhibiti bora usalama kwenye mazingira ya vurugu na mapigano. Polisi hawa wanatarajiwa kupelekwa Darfur, Sudan kulinda amani.

Mafunzo ya siku tano yamefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani na yanaendelezwa katika Taasisi ya Kofi Annan ya Kimataifa Kufunza Ulinzi wa Amani iliopo Accra, Ghana. Kadhalika, wataalamu wa Kitengo cha Polisi cha Idara ya UM juu ya Operesheni za Amani Duniani (DPKO) pia wanashiriki katika kuongoza mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha vizuri zaidi kazi za mapolisi kwenye mazingira ya uhasama. Vikosi mseto vya Shirika la UM/UA kwa Darfur (UNAMID) vinatazamiwa kupokea karibuni askari polisi 6,400 wa kimataifa watakaonezwa kwenye eneo la uhasama la Darfur, katika Sudan magharibi.