Takribani watoto milioni 4 nchini Pakistani bado wanaishi kwenye maji machafu yaliyotwama- UNICEF
Nchini Pakistani, janga la uhai wa mtoto bado ni changamoto kubwa kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko zaidi ya miezi minne iliyopita huku idadi ya maambukizi ya magonjwa ya hewa na utapiamlo uliokithiri au unyafuzi ikiendelea kuongezeka, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa inajiandaa kwa ajili ya mkutano wa kuchangia taifa hilo la Asia ili lijenge mnepo dhidi ya majanga.