Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC
Picha: MONUSCO
Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC

Amani na Usalama

Kikosi cha tisa cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania, TANZBATT 9 kinachohudumu ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, kimeanzisha kampeni iliyopewa jina la “Afya na Amani” ambayo inahusisha utoaji wa dawa za binadamu katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za baadhi ya maeneo ya uwajibikaji ya Kikosi hicho ndani ya mji wa Beni, kaskazini mashariki mwa DRC.

Akipokea dawa hizo muuguzi Mkuu wa Kituo cha afya cha Mavivi, Kisu  Kanyambala Janvier, amewashukuru TANZBATT 9 kwa msaada huo na kusema kwamba utawasaidia wananchi wote.

“Tunashukuru sana kikundi cha watanzania wa MONUSCO kwa msaada waliotuletea na ni msaada mkubwa wa dawa, tulikuwa na ulazima wa kuipata hii dawa na tulikuwa tunaikosa. Tunashukuru sana msaada huu utasaidia wakina mama, watoto na watu wote.” Anasema Kanyambala.

Aidha Kanyambala amebainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa walinda amani wa Tanzania katika eneo hilo kuwasaidia wananchi kwani waliwajengea wodi ya akina mama na watoto na ujenzi wa kantini kwa ajili ya wagonjwa kula chakula ambayo ipo mbioni kukamilika.

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC
Picha: MONUSCO
Walinda amani wa UN kutoka Tanzania waanzisha kampeni kutumia afya kuleta amani DRC

Kwa upande wake Kamanda Kikosi wa TANZBATT 9  Luteni Kanali Barakael Jackson Mley amesisitiza kuhusu suala la ushirikiano baina ya walinda amani wa MONUSCO na wananchi na kueleza kuwa wananchi wanapokuwa na afya nzuri wataweza kushiriki vyema katika kuleta amani ya maeneo yao, “sisi ujumbe wetu mkubwa ni ushirikiano ili kutatua changamoto za kiusalama tulizo nazo, bila ushirikiano baina ya raia na kikundi chetu cha tisa cha ulinzi wa Amani kutoka Tanzania hatutaweza kufanikisha jukumu hili”.

Akisisitiza umuhimu wa kampeni hiyo kwa jamii, Kavumba Dezanji ambaye ni kiongozi wa wanawake katika eneo la Mbau amesema, “nasema afya mbele ya yote, ukiwa na afya njema utafanya kazi yoyote ya maendeleo.” Aidha, Dezanji ameomba usalama uboreshwe katika eneo la Mbau na kuomba mradi kama huo wa Afya na Amani uendelee katika mji huo.

Naye Bukuka Makofi Chifu wa kimila wa eneo la Mavivi, amewashukuru walinda amani kutoka Tanzania kwa msaada huo na kusema “ni kitu cha kushukuru sana, inaonesha kama wanaendelea kutuonesha ushirikiano na upendo, mwanzo wa mwaka sisi kama tumebarikiwa kwa sababu tulikuwa na shida ya dawa kutokana na eneo hili kupokea watu wengi kutoka sehemu nyingine, hii itaendelea kutusapoti sana.”

Kampeni ya Afya na Amani ni kampeni iliyoanza kuanzia tarehe 03 mwezi huu wa Januari na itadumu hadi tarehe 13 januari 2023.