Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Sedelia Abdullahi ni mhudumu wa afya wa mstari wa mbele huko mashinani nchini Ethiopia na kila siku huchunguza na kutibu watoto wenye utapiamlo kwenye kituo cha afya cha kambi ya wakimbizi ya Bambassi nchini Ethiopia kilichojengwa na UNICEF kwa ufadhili …
UNICEF Ethiopia

Wahudumu wa afya Ethiopia warejesha tabasamu kwa watoto- UNICEF

Nchini Ethiopia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniain, UNICEF kupitia msaada kutoka Muungano wa Ulaya umewezesha mamia ya wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kila uchao kuweza kutembelea wakimbizi wa ndani waliofurushwa makwao kutokana na mzozo kwenye jimbo la Benishangul-Gumuz lililoko kaskazini-magharibi mwa taifa hilo, likipakana na Sudan ili kuwapatia huduma za lishe bora wakati huu ambapo watoto wanakabiliwa na utapiamlo.

Sauti
2'31"
Watoto wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakicheza kuruka kamba katika makazi ya wakimbizi ya Palabek Ogili nchini Uganda
© UNICEF/Jimmy Adriko

Ukosefu wa mazoezi ya mwili kichocheo cha utipwatipwa: WHO

 

Katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2020 mpaka mwaka 2030 inakadiriwa watu milioni 500 watakuwa wameugua magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari, utipwatipwa na magonjwa ya moyo kutokana na kutofanya mazoezi ya mwili, imesema ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO. 

Sauti
4'6"
Adongo Mirriam mkunga katika kituo cha Lira IV nchini Uganda akiwa na kasha la kubebea chanjo lililonunuliwa na UNICEF kwa msaada wa fedha kutoka Japan.
© UNICEF/Stuart Tibaweswa

Msaada wa UNICEF wa majokofu ya sola wawa mkombozi wa chanjo Lira Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya Japan, wanaisaidia serikali ya Uganda kuimarisha uwezo wa mfumo wa uhifadhi wa chanjo baada ya mfumo wa afya kuathirika vibaya na janga la COVID-19, lengo likiwa kuhakikisha kila mtoto na kila mtu hasa katika jamii zisizojiweza anapata chanjo za kuokoa maisha. Taarifa zaidi inasomwa studio na Happiness Palangyo wa Redio washirika Uhai FM 

Sauti
3'8"
Uchumi utokanao na shughuli zisizorasimishwa kama hapa nchini Madagascar, ni hali ya kawaida katika mazingira ambamo hakuna ajira zisizo na staha na zenye ujira mdogo
ILO/Marcel Crozet

Ukweli mchungu wakabili dunia ikiadhimisha siku ya kutokomeza umaskini- UN

Tunakabiliwa na ukweli mchungu ya kwamba dunia inarudi nyuma badala ya kusonga mbele wakati huu ambapo hii leo tunaadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii yenye maudhui, Utu kwa Wote kivitendo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Sauti
2'5"
Wanawake na watoto wakitoka kuchota maji nchini Zambia
© UNICEF/Karin Schermbrucke

Mradi wa kusoma na kuhesabu waleta manufaa kwa wanafunzi nchini Zambia

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF nchini Zambia kwa kushirikiana na serikali ya Zambia na Taasisi ya Hampel wanaendesha programu iitwayo Catch Up yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi nchini humo kupata matokeo bora ya masomo ya hisabati na kusoma hususan wale waliokuwa na ufaulu mdogo wa masomo hayo na sasa matokeo chanja yameanza kuonekana.

Sauti
2'35"
Baadhi ya matatizo ya ugonjwa wa kisukari ni upofu,kiharusi na kuharu figo.Roseane wa Brazil ana aina ya pili ya Kisukari.
WHO/Eduardo Martino

Watu bilioni 2.2 wana uoni hafifu au upofu duniani kote:WHO 

Shirika la afya duniani WHO limetoa rai ya kuhakikisha fursa ya huduma za macho zilizo bora, jumuishi na kwa wote zinapatikana wakati huu ambapo takriban watu bilioni 2.2 kote duniani wanaishi na changamoto ya uoni hafifu au upofu. Taarifa zaidi inasomwa na Happiness Pallangyo wa Radio washirika Uhai FM. 

Sauti
2'39"
Mkulima wa mwani visiwani Zanzibar nchini Tanzania
© FAO/S. Venturi

Mashirika ya UN yazindua mradi wa pamoja wa dola milioni 5 ili kuharakisha uwezeshaji wanawake Tanzania

Hii leo Jumatano visiwani Zanzibar nchini Tanzania, mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Chakula na Kilimo (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kushughulikia masuala ya wanawake, (UN Women) wamezindua programu ya miaka mitano ya kuongeza kasi ya Uwezeshaji wa mradi wa uimarishaji uchumi wa wanawake wa Vijijini. 

Sauti
4'11"
Bi. Krishnakumar Jeyaranjini, mnufaika wa mradi wa ILO wa kujengea uwezo wa kiuchumi kaya zinazoongozwa na wanawake nchini Sri Lanka hasa maeneo yaliyokuwa yameathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
ILO

Mradi wa ILO waleta matumaini kwa watamil nchini Sri Lanka

Nchini Sri Lanka, serikali na mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya amani kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO, wanatekeleza mradi wa kuinua jamii za watamil ambazo zimerejea kwenye makazi yao baada ya mzozo wa muda mrefu kaskazini mwa nchi hiyo, mradi ambao unawezesha jamii kujumuika tena na kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kuinua kipato chao baada ya mzozo uliodumu kwa takribani miaka 25.

Sauti
2'3"