Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa UNICEF wa majokofu ya sola wawa mkombozi wa chanjo Lira Uganda

Adongo Mirriam mkunga katika kituo cha Lira IV nchini Uganda akiwa na kasha la kubebea chanjo lililonunuliwa na UNICEF kwa msaada wa fedha kutoka Japan.
© UNICEF/Stuart Tibaweswa
Adongo Mirriam mkunga katika kituo cha Lira IV nchini Uganda akiwa na kasha la kubebea chanjo lililonunuliwa na UNICEF kwa msaada wa fedha kutoka Japan.

Msaada wa UNICEF wa majokofu ya sola wawa mkombozi wa chanjo Lira Uganda

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya Japan, wanaisaidia serikali ya Uganda kuimarisha uwezo wa mfumo wa uhifadhi wa chanjo baada ya mfumo wa afya kuathirika vibaya na janga la COVID-19, lengo likiwa kuhakikisha kila mtoto na kila mtu hasa katika jamii zisizojiweza anapata chanjo za kuokoa maisha. Taarifa zaidi inasomwa studio na Happiness Palangyo wa Redio washirika Uhai FM 

Eneo la Lira Kaskazini mwa Uganda ni moja ya maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa na janga la COVID-19 ambalo limeuacha hoi mfumo mzima wa afya ikiwemo huduma za uhifadhi na utoaji chanjo. 

Lakini sasa kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na shirika la UNICEF kwa ufadhili wa serikali ya Japan umerejesha matumaini ya wakazi na hususan watoto kupata chanjo wanazostahili kwani shirika hilo limenunua na kuweka majokofu maalum 115 ya kuhifadhi chanjo ya COVID-19 na kupiga jeki chanjo zingine za kawaida ambazo ni za kuokoa maisha kwa watoto.

Dkt. Ochen Buchan Patrick ni afisa wa huduma za afya wilayani Lira anasema,  “huu ni uwekezaji mkubwa ambao utatusaidia sana kutoa huduma zote muhimu kwa saa 24 bila kuingiliwa na ukarabati wa mfumo wa baridi . Mfumo huu mpya sasa unafanya kazi vizuri kwa sababu unatumia  nishati ya sola na ninafurahi kwamba sasa hatuhangaiki kugawanyaganywa gesi na kisha Kwenda kukusanya mitungi. Hivyo gharama za uendeshaji zimepungua kwa kiasi kikubwa , lakini pia mfumo wetu wa baridi wa uhifadhi umeimarika sana.” 

UN inasema mwaka 2037 idadi ya watu duniani itafikia bilioni 9
© UNICEF/Stuart Tibaweswa
UN inasema mwaka 2037 idadi ya watu duniani itafikia bilioni 9

Kabla ya mfumo huu mpya wa kuhifadhi chanjo,ilikuwa changamoto kubwa kuwafikia walengwa na chanjo muhimu kama asemavyo Mirriam Adongo afisa wa program ya chanjo katika kituo cha afya cha Ogur.

“Tulikuwa tunakwenda hadi Lira mjini kupeleka chanjo. Tulikuwa tunaendesha pikipiki hata wakati wa mvua , na chngamoto ya hali mbaya ya hewa, barabara mbaya vyote vilikuwa vinatusibu, lakini sasa kwa mfumo kuletewa hapa imefanya kuwa rahisi kwetu hata kutoka nje kwa sababu tunaweza kupata chanjo kwa urahisi na pili unatumia sola, kabla ya hapo tulipokuwa na mtambo unaotumia umeme , umeme ukikatika tu ilitulazimu kukimbiza chanjo zote hadi kwenye kituo cha wilaya cha kuhifadhi chanjo mjini ambayo ilikuwa kazi kubwa” 

Uongozi wa huduma za afya wa Lira unasema sasa huduma zimeimarika na la msingi lililosalia ni kuhakikisha vifaa hivyo  vinatunzwa vyema na kudumu kwa mufda mrefu ili kuendelea kuihamasisha jamii na kuwapa chanjo muhimu. 

Nalo shirika la UNICEF limesema furaha yake ni kuona lengo lililokusudiwa linatima kwani kwao kuwekeza katika vifaa hivyo vya mfumo wa bardidi wa kuhifadhi chanjo ilikuwa muhimu sana kama ilivyo kuwekeza kwenye upatikanaji wa chanjo zenyewe na sasa hata vituo vya afya vya vijijini kabisa vinaweza kuhifadhi chanjo zake, shukran kubwa kwa serikali ya Japan.