Haiti inaendelea kuimarika hatua kwa hatua - Lacroix
Operesheni ya usaidizi wa ujenzi mpya nchini Haiti itafanikiwa tu endapo uhusiano kati ya serikali ya nchi hiyo na na operesheni mpya ya ujenzi ukiwa mzuri.
Operesheni ya usaidizi wa ujenzi mpya nchini Haiti itafanikiwa tu endapo uhusiano kati ya serikali ya nchi hiyo na na operesheni mpya ya ujenzi ukiwa mzuri.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa ushirikiano na kampuni ya Panasonic Solar Lanterns, wametoa msaada wa umeme unaotumia nishati ya jua au wa sola kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 2400 nchini Ehtiopia.
Jumuiya ya kimataifa imechagizwa kulipa fadhila kwa Yemen ambayo imeelezwa kuwa katika zahma kubwa na janga baya zaidi la kibinadamu duniani, nchi ambayo ambayo awali iliwakarimu wageni, waomba hifadhi na hata wakimbizi, sasa imejikuta njia panda mamilioni ya watu wake wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
“Wanawake wakijengewa uwezo kiuchumi wataweza kukabiliana na matatizo mbalimbali katika jamii inayowazunguuka ikiwemo suala la tabianchi na mazingira na pia ukatili wa kijinsia”
Kamati ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa imeanza leo vikao vyake vitakavyo jadilia upokoanyaji silaha ikiwemo za nyuklia na zile za maangamizi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema taarifa za msiba wa mwanaharakati wa kupigania haki za binadamu na kupinga ubaguzi wa rangi Winnie Madikizela Mandela uliotokea mapema leo umemshitua na kumgusa sana.
Umoja wa Mataifa umepongeza na kukaribisha hatua zilizopigwa na tume huru ya uchaguzi nchini Afghanistan (IEC) kwa kupanga Oktoba 2018 kufanyika uchaguzi wa bunge na madiwani.
Makadirio ya idadi ya watakaokimbia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo (DCR), kuelekea Uganda mnamo 2018 yamepanda karibu mara nne, limesema Shirika la Umoja wa mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), nchini Uganda.
Amani na Usalama ni mambo yanayoenda pamoja na ndivyo hivyo ambavyo Umoja wa Mataifa umetumia mbinu mpya ya kuwajumuisha waendesha bodaboda huko Sudan Kusini ili wawe sehemu ya kuchagiza na kueneza amani kwenye nchi hiyo ambayo tangu disemba 2013 vuta nikuvute imeshamiri.
Usonji hukwamisha maendeleo ya mtoto na anapokuwa wa kike basi hali inakuwa mbaya zaidi.