Kazi ya kupokonya silaha si rahisi-UN

2 Aprili 2018

Kamati ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa imeanza leo vikao vyake vitakavyo jadilia upokoanyaji silaha ikiwemo za nyuklia na zile za maangamizi.

Akihutubia kikao cha ufunguzi Mkurgenzi na naibu mwakilishi wa ofisi ya  Umoja wa Mataifa inayohusika na upokonyaji silaha,Thomas Markram amesema ofisi yake inafanya juu chini kutimiza suala hilo la upokonyaji wa silaha na kuongeza kuwa

(SAUTI YA MARKRAM)

Imekuwa ikitayarisha mwelekeo wenye mkakati unaowajumuisha wote katika kuunda ajenda hii na tunafanya kila juhudi kuweza kutoa mwelekeo huo katika majira ya chipukizi”.

Mkutano huu umekuja siku chache baada ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kuonyesha wasiwasi wake kuhusu mvutano kati ya Urusi na Marekani, mataifa mawili yenye nguzu za silaha za maangamizi.

Pia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea hofu yake ya  mwelekeo wa mvutano huo kufanana kidogo na zama za vita baridi kati ya Marekani na Urusi lakini wakazi wa zama hizo pande mbili hizo zilikuwa na udhibiti wa mvutano huo.

Pia tisho lingine ni matamashi ya pande husika katika rasi ya Korea ambapo bwana Markram amesema

(SAUTI YA MARKRAM)

Miezi sita iliyopita, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alilionya baraza la usalama kuhusu tisho la matumizi ya Nuklia. Alitiwa wasiwasi na matamshi ya ugomvi katika rasi ya Korea jambo ambalo lilikuwa linaivuta hali kama kuelekea kwenye mgogoro.”

Licha ya hali kuwa ya wasiwasi kwa upande mwingine amesema kuwa kumekuwepo na ishara za maendeleo fulani ambapo shirika hilo linaweza kusaidia kutoa muongozo

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter