Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti inaendelea kuimarika hatua kwa hatua - Lacroix

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa Amani za umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Haiti.
UN Photo/Loey Felip
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa Amani za umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Haiti.

Haiti inaendelea kuimarika hatua kwa hatua - Lacroix

Amani na Usalama

Operesheni ya usaidizi wa ujenzi mpya nchini Haiti itafanikiwa tu endapo uhusiano kati ya serikali ya nchi hiyo na  na operesheni  mpya ya ujenzi ukiwa mzuri.

Hayo yamesemwa na mkuu wa operesheni za ulinzi wa Amani za umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, wakati akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu  hatua zinazoendelea Haiti.

Lacroix amelielezea baraza hilo kuhusu  ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu operesheni mpya ya ambayo itaisaidia pia Haiti kisheria ijulikanayo kama MINUJUSTH.

Bwana Lacroix amesisitiza kuwa uhusiano mzuri  kati ya pande hizi mbili unafaa uegemee mshikamano na kuaminiana ili kuweza kufanikiwa katika malengo ya kuliinua tena taifa hilo lililopitia misukosuko mingi ikiwemo tetemeko la ardhi, mlipuko wa kipindupindu n ahata hatihati ya kisiasa..

Hii ndiyo mara ya kwanza , kwa mujibu wa Larcoix, baraza linajadilia operesheni mpya ya Umoja wa Mataifa ya kusaidia Haiti kwa masuala ya kisheria, MINUJUSTH, tangu ianzishwe Oktoba mwaka jana 2017.

Pia ametaja baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kufikia sasa  katika juhudi za kuisadia  Haiti kufufua  mfumo wa sheria ikiwa ni pamoja na kubadili baadhi ya vipengele vya katiba. Ameongeza kuwa  opereshi ya sasa ya Umoja wa Mataifa inafanya kazi zake kama kawaida japo kuna matatizo ya hapa na pale.

Amesema kuwa maafisa wa kikosi hicho, raia wa kawaida, wamejikita katika mji mkuu wa Port- au -Prince huku timu zingine ndogondogo za kuhamahama zikichunguza hali ya kisiasa na  utawala wa sheria zinazurura  mikoa yote 10 huku maafisa wake wakiwasiliana na wananchi pamoja na washika dau wengine.

Pia kikosi cha Umoja wa Mataifa kimetuma maafisa wake sio tu katika vikosi vya polisi lakini pia katika magereza 18 nchini humo.

Amesema kuwa eneo ambalo wametilia mkazo ni  kusaidia  kukabiliana na watu kuwekwa ndani bila kufikishwa mahamani  na vilevile mjazo gerezani.

Hata hivyo ameongeza kuwa tatizo baado ni udhaifu katika taasisi za sheria  kuendelea kuzusha changamoto kwani kuna baadhi watu ambao hawaguswi kwa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi endapo wametenda makosa.