Wakimbizi 200,000 wa DRC, watarajiwa Uganda 2018

Wacongo wanaotoroka Vurugu DRC kuelekea Uganda. Picha: UN/John Kibego

Wakimbizi 200,000 wa DRC, watarajiwa Uganda 2018

Wahamiaji na Wakimbizi

Makadirio ya idadi ya watakaokimbia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo (DCR), kuelekea Uganda mnamo 2018 yamepanda karibu mara nne, limesema Shirika la Umoja wa mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), nchini Uganda. 

Mapema Januari, UNHCR, ilitangaza kuwa ni wakimbizi 60,000 pekee walioarajiwa huku Uganda kutoka DRC, lakini sassa kwa mshangao wao, wamepita idadi hoyo katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.

Kulingana na Afisa mwandamizi wa mawasiliano, wa UNHCR, Uganda, Joyce Muntyao-Mbithi, tayari wamesajili wakimbizi 65,773.

Sasa makadirio ya shirika hilo na wadau wake yamepanda hadi wakimbizi 200,000, mwaka huu 2018.

Bi. Munyao-Mbithi amesema tayari wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kuwahudimia, hasa katika mahitaji ya elimu na afya kwani wengi wa wanaokimbia ni watoto na wanawake.

Hivyo ameonyesha haja ya wahisani kuangalia kwa jicho la huruma, mzozo wa wakimbizi, Uganda.

Idadi kubwa yao wanakimbia wametoroka mashambulio ya kikabila jimboni Ituru na wengine ukatili unaotekelezwa katika mapambano baina ya vikundi hasimu vya wanamgambo na wanajeshi wa serikali.