Kamwe hatutowasahau wahanga wa mauaji ya maangamizi makubwa ya Holocaust: Guterres
Katika siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya maangamizi makubwa ya Holocaust Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kupitia ujumbe maalum wa siku hii amesema " leo tunawaomboleza watoto milioni 6 wa Kiyahudi, wanawake, na wanaume waliouawa katika mikono ya Manazi na washirika wao, na tunawaenzi Waroma na Wasinti, watu wenye ulemavu, na wengine wengi sana ambao waliteswa na kuuawa katika Maangamizi Makubwa ya Holocaust.