Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali ya Ukraine
UN Photo/Evan Schneider

Jitihada za Baraza la Usalama kukomesha uvamizi wa Urusi Ukraine, zakumbana na kura ya turufu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jioni hii limekutana kwa dharura kwa mara nyingine kujadili hali inayoendelea kutia wasiwasi mkubwa nchini Ukraine  kwa lengo la kuiwajibisha Urusi kuzingatia kazuni na sheria za kimataifa lakini jitihada hizo zimegonga mwamba baada ya Urusi kuamua kwa mara nyingine kutumia tena kura yake ya turufu kupinga azimio lolote dhidi yake. 

Nchini Madagaska, Rachelle Elien, afisa wa masuala ya kibinadamu wa OCHA na mwanachama wa timu ya dharura ya UNDAC, hukutana na watu walioathirika baada ya Kimbunga cha Emnati.
Chris Monnon / Atlas Logistique / OCHA

Kimbunga Emnati kuongeza zahma Madagascar:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limesema kimbunga Emnati kilichoikumba Madagascar Jumatano ya wiki hii (23/02/2022) kikiwa kimbunga cha nne kulikumba taifa hilo katika wiki kadhaa kinatishia uhakika wa chakula na ni mfano wa kjinsi gani cangamoto za mabadiliko ya tabianchi zisiposhughulikiwa zinaweza kusababisha mahitaji makubwa ya kibinadamu.