Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko ya Ziwa Albert Uganda yagharimu wilaya ya Buliisa dola 250,000

 ROSE ATIMUNEDI AKIWA AMESAKA HIFADHI KWA DADA YAKE BAADA YA NYUMBA YAKE KUHARIBIWA NA MAFURIKO.jpg
UN/ John Kibego
ROSE ATIMUNEDI AKIWA AMESAKA HIFADHI KWA DADA YAKE BAADA YA NYUMBA YAKE KUHARIBIWA NA MAFURIKO.jpg

Mafuriko ya Ziwa Albert Uganda yagharimu wilaya ya Buliisa dola 250,000

Ukuaji wa Kiuchumi

Mafuriko kwenye Ziwa Albert yamekuwa na madhara kwa uchumi kutokana na kutokea kwake wakati moja na mlipuko wa COVID-19 mwanzoni mwa mwaka 2020 hadi sasa Februari 2022.

 Athari zake kwa watu binafsi na tasisi kama zile za serikali za mitaa zimekuwa bayana. Wilaya ya Buliisa pekee imetoa takwimu zikionesha kwamba walipoteza zaidi ya shilingi bilioni moja takribani $250,000 kutokana na mafuriko yaliosababisha kuhairishwa kwa safari za kivuko cha MV Albert 1 kutoka Wanseko hadi kwneye soko la samaki la Panyimur – lililo kubwa ziadi kwenye Ziwa Albert.

Kutana na Bwana Olwinyi Mugisa, kwenye ufukwe wa Kyabarangwa wilayani Hoima anayeelezea maafa anayokumbana nayo kutokana na mafuriko. Yeyé na familia yake wamegeuka wakimbizi wa ndani wanaohifadhiwa kwenye ardhi ya jamii ya Wakibiro baada ya makaazi yake kutwama.

Kuna wengine zaidi ya 3,000 kama yeye kwenye ufukwe huu pekee.

“Mafuriko yametwamisha nyumba zangu nne pamoja na mali nyingi  sana. Mbili zilikuwa za kupangisha” asema Olwinyi.

Olwinyi alikuwa amejiimarisha katika nyanja ya uvuvi na kuanza kutumia boti la injini lakini kwa bahati mbaya injini yake inayogharimu takribani dola 2,000 kuharibiwa wakati nyumba yake ilipobomolewa na mafuriko.

ALIOKUWA MAKAAZI PASALIA MITI INAYOKAUKA BAADA YA NYUMBA KUTWAMA KWENYE UFUKWE WA bUTYABA.
John Kibego
ALIOKUWA MAKAAZI PASALIA MITI INAYOKAUKA BAADA YA NYUMBA KUTWAMA KWENYE UFUKWE WA bUTYABA.

Baadhi ya watu wa Ziwani huwa na mashamba ya mboga na viazi vitamu miongoni mwa mengine kwa ajili ya chakula na mauzo. 

Robinah Mulimba anaeleza akinyooshea kidole kwenye Ziwa pasipo na mmea wowote akikumbuka yaliokuwa mashamba.

“Haha yote unayoona yalikuwa mashamba ya viazi vitamu, maharagwe na mboga lakini sasa ni maji”, asema Mulimba.

Bwana Badru Knatanda, mkaazi wa Butyaba anasema pato lake limepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na athari za mafuriko.

Kantanda ambaye alikuwa mchuuzi mahiri wa bidhaa mbalimbali kutoka Uganda kuelekea nchi jirani ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameseam sasa anakabiliwa na kipindi kigumu kuliisha familia tofauti kabisa na wakati kabla ya mafuriko amabapo alikuwa na

alikuwa na uhakika wa pato la angalao shilling 100,000 – takribani $25 kwa siku.

“Siku hizi tunashidwa kupata hata chakula. Bishara ilikwama kabisa kwnai waliokuwa wateja wetu walipoteza makaazi na mapato yao”, asema Knatanda.

Wajasiriamali kama wafugaji wa kuku na mbuzi walipoteza mengi wakati wa pilikapilika za mafuriko hasa wakati maji yalikuwa yakiongezeka ghafla baada ya wizara ya Maji  na mazingira kuyafungua kwenye Ziwa Victoria ili kuokoa bwawa la taifa la umeme. Ziwa Victoria lipo juu kwenye mkondo wa Mto Nile nchini Uganda.

Naibu Waziri wa Mjai na Mazingira, Beatrice Anywar ameeleza kilichowasukumiza kufungua, maji kwenye Ziwa Ziwa Victoria kati ya mafuriko.

“Na tunapofungua maji hayo kwa wengi, yanatelemka kwneye mkondo wake kwa wnegi zaidi. Ndio maana madhara makubwa zaidi yanaonekana kwneye ZIwa Kyoga na ZIwa Albert. Wakazi wanjiuliyanakotoka bila nvua lakini nilazima tuyafungue ili kuokoa bwawa”, asema Anywaar.

Atimunedi Rose ni mwanamke ambaye alipoteza nyumba yake kutokana na mafuriko na sasa anahifadhiwa na dadake ambaye alikuwa na pesa kidogo za kupanga nyumba kwani naye nyumba zake zilitwama.

 Robert Mugume, diwani wa mji wa Butyaba wilayani Buliisa anasema, kukatishwa kwa huduma ya umeme kutokana na kutwama kwa nguzo za umeme kulichochea hali ya uchumi kuzorota.

“Watu walikuwa wamezoea umeme kiasi kwamba kuanzisha hata biashra ndogo ilikuwa ni rahisi kwa mfano kukata nywele. Mtu alikuwa akipanga nyumba yenye umeme tayari, lakini baada ya kukatisa huduma ya umeme ikawa inahitaji pesa nyingi kwani ni lazima ununue sola, betri na inverter amabvyo ni ghali. Biahsara nyingi zilikwama na vijana wengi sana sasa hawana akzi”, aeleza.

Hali kama hii ni dhahiri katika wilaya ya Ntoroko zaidi ya kilomita 200 kutoka hapa kama anavyoeleza idhaa hii, Mary Grace Mugasa, Naibu waziri wa huduma za umma. 

 “Tulipokwenda wialyani Ntoroko na Waziri Mkuu, tulibaini kuwa watu wengi hawafikii umeme. Unapokwenda sehemu za Butyaba unapata kwamba hawajawa na umeme kwa mwaka moja na nusu. Inamaanisha hawazalishi tena kwa mfano wale waliokuwa wakichomelea vyuma na kukata nywele. Inasumbua kabisa na imeathiri utoaji wa huduma za umma”

Familia ya wathirika wa mafuriko kwenye ufukwe wa kibiro.
John Kibego
Familia ya wathirika wa mafuriko kwenye ufukwe wa kibiro.

 Hali ya uchumi imezorota zaidi kutokana na mwendelezo wa masharti ya kudhibiti mlipuko wa COVID-19 na pia operesheni ya kupambana na uvuvi haramu. 

Bwana Mugume anasema kuwa kwa bahati mbaya vijana wengi walikuwa wakifanya uvuvi kwa kutumia nyavu zinazotambuliwa na serikali kuwa haramu kilichowapelekea kupoteza ajira mara moja baada ya kuazisha operesheni ya kupambana na uvuvi haramu ilioanza wakati hata uvuvi umevurugwa na mafuriko.

Bernard Barugahara ni Afisa wa Maendeleo ya jamii wilayani humo anasema mafuriko haya yamevuruga mipango mingi ya serikali ya kutokomeza umaskinikwani miradi nyingi ilikuwa kwenye fukwe za ziwa.

 Kwa mantiki hiyo wanapanga kudurusu baadhi ya miradi na kuhamasisha jamii upya kuona kwamba haivunjiki moyo.

“Wengi wa watu wetu walikuwa na miradi yao ya maendeelo kwenye fukwe za Ziwa. Kwanza kabisa mafuriko yalipotokea watu walilazimika kukimbia makaazi yao, mali ziliharibiwa na hata miradi yao kukwama. Baadhi ya watu walipoteza uhai wao na kwa hivyo tunajaribu kuwahamasisha watu hao na pia tunapanga kudurusu baadhi ya miradi kwani miradi kama vile uchuuzi wa samaki iliathiriwa”, asema Barugahara.

 Lakini kwa upande wake Mugume, ni vyema serikali kuu ifikirie kuwanunulia nyavu halali kwani ni njia pekee ya kukwamua uchumi wa wanaziwa hao.

 “Tuna matumaini lakini hata kama serikali ni ya kutusaidia, inapaswa kutupatia nyavu halali kwani huu ni ufukwe na pia watu wengi hutegemea uvuvi.  Ni lazima warejee kwenye kazi yao ya uvuvi ili wawe na kipato”

Na kuonesha haja ya kuhamasisha jamii katika myanja mbalimbali kwani madhara yamekuwa mtambuka. 

“Ni kwamba watu wengi hapa wanahitaji kuhamasishwa kuona kwamba wanahimili mazingira yaliopo ili waweze kuendelea. Hii ni kwa sababu sasa hivi kuna mimba za utotoni, shule ziliathirwa, hamna pesa na kwa hiyo kati ya changamoto hizi siamini kwamba ikiwa hawatahamasishwa wataweza kuendelea”  aongezea bwana Mugume.

OLWINYI MUGISA AKIWA KWENYE ARDHI YA KIJAMII YA WAKIBIRO ALIKOSAKA HIFADHI.
John Kibego
OLWINYI MUGISA AKIWA KWENYE ARDHI YA KIJAMII YA WAKIBIRO ALIKOSAKA HIFADHI.

Wizara ya maji na mazingira inaonya kuwa ingawa sasa kiwango cha maji kinapungua, mvua za Machi na April zinaweza kuchochea kiwango cha mafuriko kuliko wakati mwingine wote tangu yaanze mwaka 2020. 

Na wenyeji wanategemea simulizi za mafuriko ya mwaka 1962 kutabiri kinachofuata. 

Mfano ni Badru Knatanda anayesema kuwa kiwango cha maji haya kinaweza kutopungua sana kulingana na simulizi za waliokuwepo mwaka 1962. Anafikiri inaweza kudumu kwa miaka zaidi ya kumi yakipungua polepole na pia ikawa ndoto ya kurejea kwenye kiwango kabla ya mafuriko ya kipindi hiki.

“Tuliambiwa kuwa mafuriko ya 1962 yalipungua kwa mita mia moja kutoka ufukweni baada ya miaka kumi. Yalikuwa yamevamia makaazi ya watu katika mita 200. Kwa hiyo tunafikiri kwamba hata awamu hii, hayatapungua zaidi”, alisema Knatanda.

Uhusiano kati ya uchumi na huduma za umma umekuwa msingi wa madhara ya mafuriko kwa uchumi na makaazi kwenye Ziwa Albert.