Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa lengo la kuiwajibisha Urusi leo halijatimia hatukati tamaa: Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akizungumza na waandishi habari katika makao makuu ya umoja huo mjini New York
UN Photo/Manuel Elías
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akizungumza na waandishi habari katika makao makuu ya umoja huo mjini New York

Ingawa lengo la kuiwajibisha Urusi leo halijatimia hatukati tamaa: Guterres 

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kikao cha Baraza la Usalama kuhusu Ukraine amesema “Ingawa lengo letu halitajimia hatupaswi kukata tamaa. Ni lazima tuipe fursa amani na wanajeshi wanstahili kurejea makambini. Na viongozi kurejea kwenye njia ya majadiliano na amani.”

Guterres ameyasema hayo kufuatia hapo awali mswada wa azimio la kutaka kuiwajibisha Urusi kwa uvamizi dhidi ya Ukraine kugonga mwamba baada ya Uriusi ambayo ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama kutumia kura ya turufu kupinga azimio hilo.

UN iko mstari wa mbele kusaidia 

Katibu Mkuu amesema “Leo nchini Ukraine, licha ya changamoto za utendaji zinazoongezeka, Umoja wa Mataifa unaongeza juhudi za usambazaji wa msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na katika sehemu za Mashariki ya nchi hiyo, katika pande zote mbili za mstari wa makabiliano.” 

 Amesisitiza kuwa “Mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka na kuenea kwa saa. Raia wanakufa, huku takribani Wayukraine 100,000 tayari wameripotiwa kuyakimbia makazi yao na wengi wakivuka mpaka hadi nchi jirani, jambo linalodhihirisha hali ya kikanda ya kikanda ya mgogoro huu unaokua kwa kasi.” 

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali ya Ukraine
UN Photo/Evan Schneider
Baraza la Usalama lakutana kujadili hali ya Ukraine

Mratibu maalum kuhusu mgogoro wa Ukaraine 

Bwana Guterres amewaambia waandishi hao wa Habari kuwa “Ili kuimarisha hatua zetu, ninatangaza leo kwamba nimemteua Amin Awad, kuwa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa mgogoro wa Ukraine. Amin alifanya kazi kwa karibu nami kwa muongo mmoja kwenye shirika la UNHCR.” 

Katibu Mkuu ameongeza kuwa Amin ataongoza uratibu wa juhudi zote za Umoja wa Mataifa, ikijumuisha misaada yetu ya kibinadamu, kwa pande zote za mstitari wa makabiliano.  

Amezikumbusha pande zote zinazohusika katika mzozo huu lazima ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu na kuhakikisha usalama na uhuru wa kutembea wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wahudumu wengine wa misaada ya kibinadamu. 

“Hasa katika wakati kama huu, ni muhimu kukumbuka kwamba Umoja wa Mataifa sio tu jjengo bali ni makumi ya maelfu ya wanawake na wanaume kote ulimwenguni. Kulisha wenye njaa, kutoa chanjo kwa watoto, kuchagiza maendeleo, kulinda raia katika operesheni za ulinzi wa amani,kusuluhisha migogoro, kusaidia wakimbizi na wahamiaji, kusongesha haki za binadamu na kupigania, kufikisha na kutoa matumaini kwa mamilioni.” 

Amemalizia taarifa yake kwa kukumbusha kwamba katika ya umoja wa Mataifa imekabiliwa na changamoto siku za nyuma, lakini imesimamia misingi yake ya amani, usalama, maendeleo, haki, sheria za kimataifa na haki za binadamu. 

 “Kila wakati ambapo jumuiya ya kimataifa imeshikamana kwa pamoja maadili hayo yamedumishwa na yatadumishwa hata kwa kile kinachoendfelea leo. Ni lazima tufanye kila liwezekanalo ndani ya uwezo wetu ili yadumishwe Ukraine na kwa binadamu wote.”