Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

UNICEF inafanya kazi na serikali ya Nigeria kuhakikisha kila mtoto anapata mazingira salama ya kujifunzia.
© UNICEF/Dawali David

Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi - UNICEF

Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.

Sauti
2'58"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiwa na washiriki wengine wa tukio la Kwibuka30 wakiwasha mishumaa kukumbuka waliopoteza maisha wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika kwa siku 100 kuanzia Aprili 7, 1994
UN /Eskinder Debebe

Kwibuka30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo – Guterres

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona. 

Familia zawasili Sudan Kusini baada ya kukimbia mzozo nchini Sudan
© WFP/Hugh Rutherford

Idadi ya wakimbizi wanaovuka mpaka kutoka Sudan Kuingia Sudan Kusini yazidi kuongezeka

Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti. 

Sauti
2'42"
Uopoaji wa miili kutoka chini ya vifusi vya nyumba katika kitongoji cha Al-Nasr, mashariki mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
UN News/Ziad Taleb

Baraza la Usalama kujadili ombi la Palestina kuwa mwanachama wa UN

Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Sauti
2'24"