Tukinyamaza nani awasemee watoto wa Syria?- Blok
Syria! Syria! Syria! Bado ni kizungumkuzi, maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapitishwa lakini wahusika ni kama kusema "wameweka pamba masikioni."
Syria! Syria! Syria! Bado ni kizungumkuzi, maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanapitishwa lakini wahusika ni kama kusema "wameweka pamba masikioni."
Choo kimoja kutumiwa na watu 200, gharama ya yai moja ni dola 4, mfuko mmoja wa mkate dola 4, ni simulizi kutoka kwa wakimbizi walioweza kukimbia kutoka eneo la Ghouta Mashariki nchini Syria.
Mwaka wa 7 wa mzozo wa Syria umekamilika na sasa mwaka wa 8 umeanza na hakuna nuru ya kumalizika kwa mzozo huo, lakini bado tusikate tamaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.
Hatimaye misaada ya kibinadamu imewasili Ghouta Mashariki kiunga cha mji mkuu wa Syria, Damascus ikiwa ni ya kwanza tangu katikati ya mwezi Februari.
Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa mgogoro wa Syria kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.