Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye misaada ya kibinadamu yaingia Ghouta

Picha:WFP
Misaada ya kibinadamu ikipokelewa Syria baada ya kuwasilishwa na msafara wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la hilal nyekundu la Syria, SARC(Maktaba).

Hatimaye misaada ya kibinadamu yaingia Ghouta

Msaada wa Kibinadamu

Hatimaye misaada ya kibinadamu imewasili Ghouta Mashariki kiunga cha mji mkuu wa Syria, Damascus ikiwa ni ya kwanza tangu katikati ya mwezi Februari. 

Hii ni kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP kupitia ujumbe wake  kwenye mtandao wa  kijamii wa twitter ambao unaonyesha msusruru wa magari ya shirika hilo yakiingia katika eneo hilo ambalo bado linazingirwa na waasi. Msafara huo unapelekwa ni wa chakula pamoja na vitu vingine vya msingi kwa ajili ya watu takriban elfu 27 na nusu.

Jana Jumapili Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada ulimesema uko tayari kupeleka msaada Ghouta mashariki  kuanzia leo jumatatu na shehena imeshajazwa katika malori 46 ikiwemo lishe kwa watoto na vifaa vya afya.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria na mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Ali Al-Za’tari jana amesema  kikosi chake kiko  tayari kwa kazi hiyo.

Eneo la Ghouta Mashariki limeelezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonnio Guterees kama  ni jahanamu duniani, limekuwa likizingirwa  na majeshi ya serikali kwa muda mrefu , likiwa na takriban watu 400,000.

Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema UN pamoja na washirika wake wamepokea ruksa ya kupeleka misaada kusaidia watu 70,000 mjini Duma na kuongeza kuwa  misaada iliyosalia itapelekwa huko machi nane.