Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sudan Kusini

Watoto wakimbizi wa ndani huko Ituri nchini DRC.
UN/Eskinder Debebe

Mauaji na utekaji nyara wa watoto kwenye maeneo ya vita vilishamiri mwaka 2021- Ripoti

Mwaka wa 2021  umeshuhudia mchanganyiko wa mwendelezo hatari wa mizozo, mapinduzi ya kijeshi sambamba na mizozo mipya na ile iliyodumu muda mrefu na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, vyote ambavyo kwa pamoja vimekuwa na madhara makubwa kwa watoto duniani kote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ripoti yake ya mwaka kuhusu Watoto kwenye mizozo ya kivta, ripoti ambayo imechapishwa hii leo.

Mjane raia wa Sudan Kusini ambaye mume wake aliuawa siku moja baada ya yeye kujifungua mtoto wao wa mwisho sasa ndio pekee anaihudumia familia yake
WFP/Gabriella Vivacqua

UNMISS yaendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji katika eneo la makutano la  Aru jimboni Equatoria ya Kati ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaandaa wananchi kujilinda kwa kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikijirudia na kuathiri zaidi wanawake na wasichana.