UNMISS yapongeza hukumu kwa waliotenda utakili nchini Sudan Kusini

Familia za waliokimbia makaiz yao sababu ya machafuko wakiwa wamepata hifadhi huko Tambura nchini Sudan Kusini
UNMISS
Familia za waliokimbia makaiz yao sababu ya machafuko wakiwa wamepata hifadhi huko Tambura nchini Sudan Kusini

UNMISS yapongeza hukumu kwa waliotenda utakili nchini Sudan Kusini

Haki za binadamu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS umekaribisha hatua zilizochukuliwa na serikali ya Sudan Kusini za kufuatilia na kutaka uwajibikaji kwa manusura wa ukatili wa kingono huko Yei, jimboni Equatoria ya kati. 

Taarifa ya UNMISS kutoka Juba nchini Sudan Kusini imesema mahakama Kuu ya kijeshi ya nchi hiyo iliyokaa kati ya tarehe 01 mpaka 27 mwei Juni mwaka huu wa 2022 imewatia hatiani watu 21 kwa makosa ya mauaji, ubakaji pamoja na ubakaji wa watoto wadogo makosa yaliyofanywa mwaka 2021 na 2022. 

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom amesema “Tunapongeza mamlaka na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini SSPDF kwa kuwawajibisha wahalifu kwa uhalifu wa kutisha uliofanywa. Jamii imekuwa na mchango muhimu kwani wao ndio waliotaka kesi hizi zichunguzwe na kutolewa maamuzi.”

Miongoni mwa waliochukuliwa hatua ni pamoja na wanajeshi watano wa jeshi la SSPDF waliotuhumiwa kwa ubakaji ambao walitiwa hatiani , kuvuliwa vyeo vyao, kufukuzwa kazi, kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10 jela na kulipa fidia kwa walionusurika.

Uthibitisho wa hukumu hizi unatarajiwa kufuata kwa mujibu wa sheria za jeshi la ukombozi la watu wa Sudan.