FAHAMU UMOJA WA MATAIFA
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha miezi 6 iliyopita nchini Sudani Kusini zimeathiri miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege huku zaidi ya wakazi 700,000 wa kaunti ya Maban jimboni Jonglei wakisalia wakiiishi bila kupata msaada wowote kutokana na eneo lote kujaa maji.
Licha ya kutiwa saini kwa makubaliano mapya ya amani nchini Sudan Kusini mwaka 2018, mapigano bado yanaendelea katika maeneo tofauti tofauti nchini humo ikiwemo mji wa Tambura jimboni Equatoria Magharibi na hivyo kukwamisha harakati za kufikisha huduma za matibabu na wakimbizi wa ndani kuzidi kutaabika.
Nchini Sudan Kusini wakati sasa milio ya risasi inaweza kuwa imepungua katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, jinamizi la vita vya wenyewe kwa wenyewe bado linawaandama hasa kwa kuzagaa kwa manbaki ya silaha za vita kama mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya mlipuko, ambavyo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayochukua hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS ni tishio la kila siku kwa maisha ya wanawake, watoto na wanaume kwenye maeneo mbali mbali nchini humo