Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Charlotte Fatuma, mkimbizi kutoka DRC anaendesha duka kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Coranne nchini Msumbiji kutokana na umeme ambao umefanikishwa na mradi unaotekelezwa na UNHCR, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika.
UNHCR Video

Utu na maendeleo vyakutanishwa Coranne na kuleta ustawi kwa wakimbizi na wenyeji

Charlotte Fatuma na Neema Cenga ni wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na sasa wanaishi ukimbizini nchini Msumbiji katika jimbo la Nampula. Kwa sasa Charlotte ni mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, akiendesha biashara ya duka kwenye makazi ya wakimbizi ya Coranne huku Neema naye akijitahidi kulea na kusomesha watoto wake.  

Sauti
4'28"