Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jiji la Kampala laendesha kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Ebola

Paulina Ajello mfanyakazi wa WHO kitengo cha mawasiliano na ushirikishaji jamii akizungumza na wanajamii waelimishaji kuhusu Ebola.
Picha: WHO_Uganda/PhilipKairu
Paulina Ajello mfanyakazi wa WHO kitengo cha mawasiliano na ushirikishaji jamii akizungumza na wanajamii waelimishaji kuhusu Ebola.

Jiji la Kampala laendesha kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Ebola

Afya

Wakati huu ambapo hakuna mgonjwa mpya wa Ebola aliyesajiliwa katika mji mkuu wa Uganda tangu tarehe 14 Novemba, 2022 mamlaka ya afya ya Mji Mkuu wa Kampala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya nchi hiyo hivi karibuni ilifanya kampeni ya siku saba kuelimisha umma ili kudumisha umakini wa watu na hatimaye kusaidia kumaliza mlipuko wa ugonjwa huo hatari duniani.

Kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, mamlaka ya jiji ilifanya kazi na zaidi ya wahamasishaji wa kijamii 1500 madereva wa pikipiki maarufu kama "boda boda" ambao walikwenda nyumba kwa nyumba kila siku kuhamasisha, kupambana na taarifa potofu na uvumi na kuhakikisha kuwa watu wanaripoti wale wote wanaoshukiwa kuwa vya Ebola.

Jiji la Kampala, lenye takriban watu milioni 1.5, limesajili jumla ya wagonjwa 18 tangu Uganda itangaze mlipuko wa virusi vya ebola aina ya Sudan mnamo tarehe 20 Septemba 2022. Miongoni mwa sababu zinazoelezwa kusaidia kuzuia usambaaji haraka wa ugonjwa huo katika mazingira hayo ya mjini ni pamoja na ufuatiliaji wa haraka wale wote waliokuwa wakishukiwa kuna na ugonjwa huo au kukutana na mtu aliyeshukiwa kuwa na ugonjwa huo ambapo waliweza kutengwa kwa haraka.

Ni asubuhi na mapema, wahamasishaji wapatao 150 wanakusanyika katika chumba kikuu cha Shule ya Msingi ya Nakivubo Blue, katika mojawapo ya vitongoji vya jiji la Kampala vilivyo na watu wengi zaidi. Leo, watatembea katika mitaa ya Kisenyi, eneo lenye watu wengi jijini humo, ili kushirikisha na kuhamasisha watu kuhusu mlipuko wa Ebola. “Jukumu lako ni kueneza ukweli. Tunataka kuwakumbusha watu kwamba Ebola ni kweli na bado ipo,” aeleza Pauline Ajello, afisa wa mawasiliano ya hatari wa WHO na ushiriki wa jamii.

Zikiwa zimepita zaidi ya wiki nne baada ya kuripotiwa mgonjwa wa mwisho na kuthibitishwa kuwa na Ebola katika jiji hilo, watu wengi wanadhani mlipuko huo umekwisha. Mamlaka ya afya ya Kampala, kwa ushirikiano na Wizara ya Afya na kwa msaada wa WHO, inaendesha kampeni hii ili ya uhamasishaji ili kuhakikisha kuwa umma unaendelea kuzingatia hatua za kujikinga.

Claire Arinaitwe mmoja ya waelimishaji kuhusu Ebola kutoka Kijiji cha Kisenyi
WHO_Uganda/PhilipKairu
Claire Arinaitwe mmoja ya waelimishaji kuhusu Ebola kutoka Kijiji cha Kisenyi

Wakiwa na vipeperushi na mabango, wahamasishaji wana jumuiya wanagawanyika katika vikundi vidogo na kwenda kwenye eneo walilopangiwa.

Claire Arinaitwe ni mwanachama wa Timu ya Afya ya Kijiji huko Kisenyi. Yeye na timu yake ya watu wanane wamefahamishwa kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kushughulikia uvumi.

“Baadhi ya watu wanafikiri kwamba Ebola haipo au hawana taarifa nyingi kwa sababu hawatazami TV au kusikiliza redio,” anasema, huku kila mwanachama wa timu yake akichukua sehemu ya nyenzo za mawasiliano nakuzibeba tayari kwenda kuelimisha umma.

Arinaitwe akielimisha jamii kuhusu Ebola
Picha: WHO_Uganda/Philip Kairu
Arinaitwe akielimisha jamii kuhusu Ebola

“Tunawaambia watu katika jamii kwamba Ebola inaua. Tunawaambia kuhusu ishara na dalili. Tunawaambia jinsi wanavyoweza kuepuka. Tunawaambia wanachohitaji kufanya wanapopata watu wagonjwa katika jamii,” anasema Arinaitwe.

Majibu madhubuti yaliyowekwa na mamlaka ya afya ya kitaifa na mitaa yameruhusu kudhibiti kuenea kwa virusi kwa sasa. Chakusahangaza, imetoa mtazamo kana kwamba ugonjwa huo sio tishio kubwa, hata zaidi baada ya miaka miwili mirefu ya kukabiliana na janga la coronavirus">COVID-19.

Arinaitwe na timu yake wanasimama kwenye duka la Charles Atoba kutoa elimu kuhusu Ebola
Picha: WHO_Uganda_Philip Kairu
Arinaitwe na timu yake wanasimama kwenye duka la Charles Atoba kutoa elimu kuhusu Ebola

Arinaitwe na timu yake wanasimama kwenye duka la Charles Atoba katika kitongoji chenye shughuli nyingi, cha watu wa kipato cha chini. Wapita njia nao wanasimama ili kusikiliza mazungumzo ambayo Arinaitwe anafanya na muuza duka.

“Mjini Kampala, kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu Ebola”, anasema Atoba, ambaye anakiri kutokuwa na uelewa mzuri kuhusu jinsi Ebola inavyoenea. “Lazima tusikilize watu wanaotufundisha kuhusu ugonjwa huo na lazima tuoneshe mabango yao kwenye maeneo ya umma ili watu waweze kusoma na kujua kinachoendelea.”

"Ebola bado ipo," mhamasishaji wa jamii akizungumza kwa sauti ya juu kupitia kipaza sauti.
Picha: WHO_Uganda/Philip Kairu
"Ebola bado ipo," mhamasishaji wa jamii akizungumza kwa sauti ya juu kupitia kipaza sauti.

Mbali na Timu za Afya za Vijiji na wahamasishaji wa kijamii, kampeni inategemea "boda boda". Kama nyuki kwenye mzinga, madereva hawa wa kukodi wako katika kila barabara ya jiji kuu la Kampala, wakisafirisha abiria kutoka wilaya hadi wilaya. Kama vile wakati wa janga la COVID-19, wanachukua jukumu muhimu katika kampeni ya uhamasishaji ya wiki nzima, wakiendesha pikipiki na mabango  kusambaza vipeperushi.

"Ebola bado ipo," mhamasishaji wa jamii akizungumza kwa sauti ya juu kupitia kipaza sauti.

"Ebola bado ipo," mhamasishaji wa jamii akizungumza kwa sauti ya juu kupitia kipaza sauti.
Picha: WHO_Uganda/Philip Kairu
"Ebola bado ipo," mhamasishaji wa jamii akizungumza kwa sauti ya juu kupitia kipaza sauti.

“Shirika la Afya Ulimwenguni lilitupa vipeperushi vya Wizara ya Afya na nambari ya simu ambayo inaweza kutusaidia ikiwa tutakuwa tumekutana na mtu (mwenye dalili za Ebola). Ni nambari isiyolipishwa. Unapiga simu, unaeleza wasiwasi wako na unapata usaidizi,” anasema Imam Katongol, mwendesha bodaboda huko Kisenyi.

Akiwa amerudi kutoka kwa safari ndefu katika kitongoji hicho, anasema: “Sisi kama waendesha boda boda tuko mstari wa mbele (kuathiriwa na Ebola). Tunatangamana na watu wengi, tunabadilishana pesa, wateja wengine wanatokwa na jasho… Kwa hivyo tunafanya hivi ili kuhakikisha kuwa huu (mlipuko wa Ebola) unakamilika.”