Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Burundi Ezechiel Nibigira akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74.
UN Photo/Cia Pak

Burundi yataka iondolewe kwenye ajenda ya Baraza la Usalama

Mjadala mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 ukitamatishwa hii leo  jiijni New York, Marekani, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Burundi Ezechiel Nibigira amehutubia jukwaa hilo akitaka ajenda ya Burundi kwenye Baraza la Usalama iondolewe kwa kuwa hali ya usalama nchini humo ni tulivu.

Majengo marefu na majengo ya hoteli huko Punta Pacifica, Jiji la Panama, Panama, jiji lenye moja kati ya sekta kubwa za benki katika Amerika Kati.
World Bank/Gerardo Pesantez

Benki zenye thamani ya Dola trilioni 47 zapitisha kanuni mpya endelevu zinazoungwa mkono na UN

Maendeleo ya kiuchumi

Benki, kwa pamoja, zenye mali ya thamani ya dola trilioni 47, au theluthi ya sekta nzima kimataifa, jumapili zimetoa ahadi ya kuunga mkono kanuni mpya za benki zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kukuza hatua dhidi ya tabianchi na mabadiliko kutoka mifano ya ukuaji wa uchumi "wa udhurungi hadi kijani".

Mtoto akiwa amebebwa na mamamke katika kituo cha afya nchini Mali.
UNICEF/UN0186355/Njiokiktjien

Watu bilioni 5 wakitarajiwa kukosa huduma za afya, UN kufanya mkutano wa kuchagiza huduma kwa wote

Watu bilioni 5 duniani wako hatarini kukosa huduma za afya ifikapo mwaka 2030 endapo nchi hazitochukua hatua kuziba mapengo ya upatikanaji wa huduma za afya imesema ripoti mpya iliyotolewa leo Jumapili, wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa kufanya mkutano wa kihistoria ili kuchagiza mchakato wa haraka kuhusu huduma za afya kwa wote.