Mtoto akiwa amebebwa na mamamke katika kituo cha afya nchini Mali.

Watu bilioni 5 wakitarajiwa kukosa huduma za afya, UN kufanya mkutano wa kuchagiza huduma kwa wote

UNICEF/UN0186355/Njiokiktjien
Mtoto akiwa amebebwa na mamamke katika kituo cha afya nchini Mali.

Watu bilioni 5 wakitarajiwa kukosa huduma za afya, UN kufanya mkutano wa kuchagiza huduma kwa wote

Afya

Watu bilioni 5 duniani wako hatarini kukosa huduma za afya ifikapo mwaka 2030 endapo nchi hazitochukua hatua kuziba mapengo ya upatikanaji wa huduma za afya imesema ripoti mpya iliyotolewa leo Jumapili, wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa kufanya mkutano wa kihistoria ili kuchagiza mchakato wa haraka kuhusu huduma za afya kwa wote.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, utafiti wa ripoti hiyo “huduma ya msingi ya afya kuelekea huduma ya afya kwa wote  unakadiria kwamba takriban maishja ya watu milioni 60 yanaweza kuokolewa kwa kuongeza matumizi ya huduma za msingi za afya katika nchi za kipato cha chini na cha wastani kwa dola bilioni 200 kila mwaka.”

Japo kwa ujumla huduma za afya zimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2000, ripoti hiyo ya huduma za afya kwa wote (UHC) inaonyesha  pengo kubwa la huduma za afya katika nchi masikini na zile zinazokabiliwa na vita. Maeneo ya vijijini ndio yana kawaida ya kuwa na huduma hafifu za afya kutokana na miundombinu mibovu , upungufu wa wafanyakazi na huduma dunia za afya.                                                                                                                                                                                                                                                                               

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kwamba “endapo tuko makini tunataka kufikia huduma za afya kwa wote na kuboresha Maisha ya watu ni lazima tuonyeshe dhamira ya kuhudu huduma za afya za msingi.”

Ameongeza kuwa “Hii inamaanisha kutroa huduma muhimu za afya kama vile chanjo, huduma ya mama na mtoto, ushauri kuhusu mfumo wa Maisha na kuhakikisha kwamba watu hawalipii huduma hizi kutoka mifukoni mwao.”

Ripoti hiyo imetolewa kabla ya mkutano wa kwanza kabisa wa ngazi ya juu kuhusu huduma za afya kwa wote UHC, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambao utafanyika Kesho Jumatatu ukiwa ni mkutano mmoja kati ya mikutano 5 ya ngazi ya juu itakayofanyika katika wili ya kwanza ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa unasema mkutanop huo ni mkutano muhimu sana wa kisiasa kuwahi kufanyika kuhusu mada hiyo na kushirikisha wawakilishi kutoka katika mashirika mbalimbali ikiwemo wakuu wan chi na serikali, wabunge, maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa asasi za kiraia , viongozi kutoka sekta ya biashara na wanazuoni.

Mhudumu wa afya nchiini Malawi akitoa damu ya mgonjwa kwa ajili  ya kuchunguza Malaria.
© UNICEF/Arjen van de Merwe
Mhudumu wa afya nchiini Malawi akitoa damu ya mgonjwa kwa ajili ya kuchunguza Malaria.

Afya na maendeleo endelevu SDGs

Shirika la WHO ambalo linabeba jukumu kubwa katika kuzisaidia nchi katika utekelezaji wa huduma za afya kwa wote linaamini kwamba afya ni muhimu kwa ajili ya maendeleo endelevu na limeshirikiana na serikali ya Kenya kuzindua mpango wa majaribio wa huduma za afya kwa wote katika kaunti mbalimbali ambazo zimechaguliwa kutokana na kiwango kikubwa cha magonjwa ya kuambukiza , idadi kubwa ya watu, idadi kubwa ya vifo vya kina mama na watoto, na idadi kubwa ya matukio ya majeruhi wa ajali za barabarani.

Lengo la mpango huo wa mjaribio ni kuboresha huduma za afya kwa kufuta gharama katika vituo vya afya vya mashinani na kuanzisha mfumo wa bima ya afya za jamii. Katika moja ya kaunti hizo ya Makueni , wakaazi wamekumbatia mpango huo na faraja ya moyo na akili kutambua kwamba hawatokuwa na msongo au hofu ya gharama za matibabu.

Muhitasari wa mkutano wa UHC

  • Mkutano wa UHC ni moja ya mikutano 5 rasmi na ya ngazi ya juu itakayofanyika wakati wa wiki ya mjadala wa Baraza Kuu wa wakuu wa nachi na serikali
  • Umoja wa Mataifa unauona mkutano huo kama ni muhimu sana wa kisiasa kuwahi kufanyika kuhusu UHC
  • Washiriki watakuwa ni pamoja wa wakuu w anchi na serikali , wabunge, maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa , wajumbe wa asasi za kiraia , viongozi wa sekta na makampuni ya biashara na wanazuoni.