27 Septemba 2019

Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali ni miongoni mwa waliokusanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Septemba 27 kushiriki mkutano maalum wa tathimini ya hatua zilizopigwa na nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) akiwemo Rais wa Ireland, Kenya na waziri mkuu wa Fiji na Norway.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Mkutano huu wa siku moja wa ngazi ya Juu kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu unaangalia hatua iliyopigwa na nchi za SIDS kushughulikia vipaumbele vya mataifa hayo kupitia utekelezaji wa mchakato wa SAMOA ambao ulipitishwa mwaka 2014.

Katika mkutano huo ambao unatarajiwa kutoka na azimio lililoafikiwa na nchi zote wanachama Guterres amesema “nchi za SIDS ni miongoni mwa nchi zizlizo katika hatari kubwa duniani, zikikabiliwa na changamoto za kipekee zinazohisiana na kwanza ukubwa wake, mahali vilipo visiwa hivyo, kuwa hatarini kutokana na mtikisiko wa kiuchumi nje na changamoto za kimazingira ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.”

Kinachohitajika kufanyika

Katibu Mkuu amesema mbali ya hatua zilizopigwa ni muhimu kutathimini changamoto zilizopo na katika kusonga mbele, “natoa wito kwa serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na wanazuoni kuzindua ushirika mpya kuhusu utekelezaji wa maeneo yaliyopewa kipaumbele.”

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba,“katika miaka mitano ijayo ya utekelezaji ni lazima kutafuta mwingiliano na ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu, ajeanda ya mabadiliko ya tabianchi na michakato mingine ya kimataifa. Mkutano huu unakusudia kuidhinisha "taarifa fupi ya kisiasa yenye mwelekeo na ushirikiano baina ya serikali."

Vipaumbele

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni waziri wa Sao Time na Principe wa  mambo ya nje , ushirikiano na jamii , Elisa Teixeira de Barros Pinto ambaye ameiambia UN news kuhusu haja ya visiwa hivyo vidogo vinavyoendelea . amesema moja ya vipaumbele view ufafanuazi wa maana ya uwekezaji.” Kama nchi inayoendelea yenye matarajio ya hali ya juu,nadhani jumuiya ya kimataifa kidogo imeghafirika. Imeghafirika kwa sababu rasilimali zinapelekwa kwa vitu ambavyo si vya muhimu sana , ambapo wamejikita zaidi na kupunguza umasikini, ukimwi katika sehemu mbalimbali za dunia. Na unapaswa kuangalia duniani kote na kuliona hilo na ukweli kwamba ubaguzi bado upo kwa kiasi kikubwa, pengo la usawa linaongezeka na ni pengo hili la usawa ambalo linasababisha kusiwe na haki  na kuzusha migogoro duniani.”

Mkutano huu umekuja miaka mitano baada ya makubaliano kupitishwa kusaidia maendeleo endelevu katika nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea (SIDS) makubaliano yaliyoitwa mchakato wa SAMOA. Wengine waliozungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na Rais wa Baraza Kuu Tiijani Muhammad-Bande , marais wa Ushelisheli, , waziri mkuu wa Barbados, Fiji, Samoa, Aruba, Antigua, Barbuda na Curacao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud