Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Melen, eneo la makazi duni katikati ya mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé

Miji kote ulimwenguni ni ‘sababu kuu ya mabadiliko tabianchi’- UN-Habitat

© UN-Habitat/Kirsten Milhahn
Melen, eneo la makazi duni katikati ya mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé

Miji kote ulimwenguni ni ‘sababu kuu ya mabadiliko tabianchi’- UN-Habitat

Tabianchi na mazingira

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat Maimunah Mohd Sharif, miji kote ulimwenguni ni ‘sababu kuu ya mabadiliko tabianchi’ ingawa pia inaweza kuwa na suluhisho la kupunguza hewa chafuzi gesi, ambazo zinasababisha joto ulimwenguni kuongezeka.

Bi. Sharif ataungana na viongozi wa ulimwengu katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini  New York wiki ijayo katika Mkutano wa tabianchi ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

UN-Habitat inaunga mkono moja ya hatua tisa zilizochaguliwa na Katibu Mkuu ambazo ni "Miundombinu, Miji na hatua za Mitaa" chini ya uongozi wa serikali za Kenya na Uturuki.

UN News imepata fursa ya kumhoji Bi. Sharif kuhusu mchango wa miji katika kupunguza mabadiliko ya tabianchi ambapo amesema kwamba, “zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni wanaishi mijini,  Miji hii hutumia kiasi kikubwa cha usambazaji wa nishati ulimwenguni na inasababisha karibu asilimia 70 ya uzalishaji wa gesi unaozingatia gesi chafu duniani ambazo zinasababisha joto la dunia. Viwango vya hewa ya kaboni, hewa chafuzi iko katika viwango vya juu kabisa, sana sana kwa ajili ya kuchomwa kwa mafuta ili kupata nishati.”

Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat Maimunah Mohd Sharif (wa 2 kushoto) na wanawake aliokutana nao wakati wa ziara yake katika nyumba mpya ya makazi ya UN-Habitat huko Turkana, Kenya. UN-Habitat / Julius Mwelu
UN-Habitat/Julius Mwelu
Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat Maimunah Mohd Sharif (wa 2 kushoto) na wanawake aliokutana nao wakati wa ziara yake katika nyumba mpya ya makazi ya UN-Habitat huko Turkana, Kenya. UN-Habitat / Julius Mwelu

Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat Maimunah Mohd Sharif (wa 2 kushoto) na wanawake aliokutana nao wakati wa ziara yake katika nyumba mpya ya makazi ya UN-Habitat huko Turkana, Kenya. UN-Habitat / Julius Mwelu

Bi. Sharif alisisitiza kuwa ingawa miji ndio sababu kuu ya mabadiliko ya tabianchi, pia ndio inayoathiriwa zaidi kwani miji mingi ipo karibu na maji hivyo kuwa katika hatari ya kuongezeka kwa vina vya bahari na dhoruba.

Akaongeza kwamba,“kwa kuzingatia jukumu la miji kama viboreshaji vya uvumbuzi na ubunifu, pia tunaitegemea kutupatia majibu. Nishati, ujenzi, suluhisho za mipango na uvumbuzi katika miji zina uwezo wa kupunguza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.”

Miji inawezaje kuchangia kupunguza mabadiliko ya tabianchi?

Katika suala la kupunguza gesi hatarishi, tunaweza kufaulu tukibadilisha jinsi tunavyopanga, kujenga, kusimamia na kudhibiti miji yetu.

Miji iliyoundwa vizuri, thabiti, yenye usafiri mzuri wa umma hupunguza kiwango cha kaboni na ni muhimu kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambayo hatua ya tabianchi imepewa  umuhimu.

“Tunahitaji kupunguza haraka kiasi cha kaboni dioksidi zinazozalishwa na nyumba na ofisi zetu kwa kuhamia majengo ambayo hayatumii kaboni yoyote iwe kwa taa, kupasha baridi au umeme. Wanaweza kudhibiti hii kwa kuwa na ufanisi zaidi wa nishati na kutumia vyanzo vya nishati mbadala.” Anasisitiza.

Pia, usafiri hutoa idadi kubwa ya uzalishaji. Mahitaji ya Miji hayafai kupangwa kwa kuzingatia magari ila kwa kuzingatia watu na uwekezaji uwe katika usafirishaji wa umma usiotumia kaboni, njia za miguu na njia za baiskeli zilizolindwa. Usafirishaji ambao ni wa umeme na ambao unatumia nishati mbadala vinaweza kuzuia tani milioni 250 za uzalishaji wa kaboni ifikapo 2030, pamoja na kuboresha afya ya watu, na kupunguza kelele na uchafuzi wa hewa katika miji yetu.

Taka hutoa gesi ya methano yenye nguvu zaidi kuliko kaboni kwa kiwango kifupi, kwa hivyo ni muhimu kupunguza taka za kikaboni kwa kuboresha njia za usimamizi wa taka na kuchukua hatua za kukusanya na kutumia uzalishaji wa methano kutoka taka za ardhini.

“Sisi sote tunaweza pia kuchangia katika suluhisho za muda mrefu kwa kufanya chaguzi za kibinafsi kubadilisha mitindo yetu ya maisha na mitindo ya matumizi.”

Mabadiliko ya tabianchi tayari yanafanyika na yanaathiri miji, ni kwa njia ipi miji inaweza kujiandaa kwa ukweli huu mpya?

Athari za mabadiliko ya hivi karibuni katika sayari na tabianchi, na vile vile hatari zinazotarajiwa za siku za usoni zimesukuma karibu miji elfu moja kutangaza dharura ya tabianchi.

Eneo la makazi duni huko Port-Au-Prince, Haiti
UN-Habitat/Julius Mwelu
Eneo la makazi duni huko Port-Au-Prince, Haiti

Makazi duni huko Port-Au-Prince, Haiti. UN-Habitat / Julius Mwelu

“Makazi stahimilivu yatafanya kazi tu ikiwa tunazo jamii zinazostahimili. Hivi karibuni nimekutana na Katibu Mkuu wa jumuiya ya madola, Patricia Scotland, na viongozi wengine wa ulimwengu na tumejitolea kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunarejesha maendeleo zaidi. Kuzingatia kwetu kwa "Miundombinu, Miji na hatua za Mitaa" ni sehemu ya Mpango wa Mkakati wa UN Habitat wa kujenga uvumilivu wa tabianchi ulimwenguni .

Watu maskini zaidi na walio katika mazingira magumu wameathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika miji kwa kiwango kipi?

Sehemu maskini katika miji yetu na jamii ndizo zitakazoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi kwa njia ya mafuriko, maporomoko ya ardhi na joto kali.

Hii ni kwa sababu mara nyingi wanaishi katika makazi duni katika maeneo dhaifu kama pande za mlima au maporomoko, ambako hakuna miundombinu ya kupunguza hatari kama vile mitaro ya kupitisha maji. Ulimwenguni kote, inakadiriwa kuna wastani wa watu milioni 880 wanaoishi katika makazi ambayo yako hatarini sana kuathirika kutoka na  mabadiliko ya tabianchi.

Changamoto zinakabiliwa na miji katika nchi zinazoendelea zinalinganishwa vipi  changamoto za miji katika nchi zinazoendelea?

Dunia yote inatishiwa na mabadiliko ya tabianchi lakini nchi zinazoendelea mara nyingi uhisi athari zaidi. Mara nyingi hazina uwezo wa kukabili matukio ya hali ya hewa kali na wana mfumo duni wa utawala kusimamia changamoto za tabianchi.

Pia, miji katika nchi zinazoendelea pia inakabiliwa na vizuizi katika upatikanaji wa fedha za tabianchi ikiwa ni pamoja na kutozingatia miji kama kipaumbele cha kimkakati. Mabadiliko ya tabianchi hayaheshimu mipaka yanaathiri sisi sote na tunahitaji kuchukua hatua kwa pamoja kuizuia sasa.