Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watumishi wa umma wapongezwa na UN kwa huduma na mchango muhimu

E-Thuto, Botswana mshindi wa tuzo ya watumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa UNPSA 2020
e-Thuto, Botswana, 2020 UNPSA wi
E-Thuto, Botswana mshindi wa tuzo ya watumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa UNPSA 2020

Watumishi wa umma wapongezwa na UN kwa huduma na mchango muhimu

Afya

Wakati dunia ikiendelea kupambana na janga la corona au COVID-19 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amewaenzi watumizi wa umma walio mstari wa mbele katika kupambana na janga hili na pia kwa huduma yao ya muhimu kwa binadamu.

Guterres amewapa pongezi hizo wakati leo ikiadhimishwa siku ya utumishi wa umma duniani na pongezi hizo amezielekeza kwa

“Wauguzi, madaktari na wahudumu wa afya ambao hutoa huduma ya kuokoa Maisha , wafanyakazi wa usafi ambao husafisha maeneo ya umma, wanaohudumua katika sekta ya usafiri  na kuhakikisha mabasi na treni zinaendelea kutoa huduma kote duniani, waalimu na maafisa wa afya ya umma, wakusanya takwimu na mameneja ambao hutoa taarifa muhimu kuhusu maambukizi  na jinsi ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema mara nyingi watumishi hawa wa umma hufanya kazi katika mazingira ya hatari na kukutana na wat una bila hata fursa ya kuwa na vifaa vya kujilinda na wengine wamepoteza Maisha yao kwa COVID-19 wakiwa katika harakati zao za kutoa huduma.

HYO Policy, kutoka Jamhuri ya Korea mshini wa tuzo ya watumishi wa Umma UNPSA 2020
HYO Policy, Republic of Korea, 2
HYO Policy, kutoka Jamhuri ya Korea mshini wa tuzo ya watumishi wa Umma UNPSA 2020

Wakati akiwaenzi watumishi hao muhimu Guterres ameelezea umuhimu wa kuwalinda, kuwatambua na kuwekeza katika ustawi wa watumishi hao. “Na ninasema moja kwa moja kwa watumishi hawa wa umma ambao ni mfano wa kuigwa, kwamba sote tuna deni kwenu.”

Tuinue ari ya watumishi wa umma

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tiijani Mohammed- Bande amewaambia wajumbe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo kwa njia ya mtandao kwamba “siku hii inatoa fursa ya nadra ya kujadili jinsi gani ya kujipanga serikali na huduma za umma ili kudhibiti janga hili la corona na vitisho vingine vya usalama wa umma katika siku za usoni.”

Ameongeza kuwa “ Katka kutekeleza kazi zao na kitimiza wajibu wao sekta ya umma lazima iongozwe kila wakati na misingi imara ya uongozi, maadili, kujitolea, ubora , utu, kuchukua hatua na uwajibikaji.”.

Amesema kuwa katika kudhiditi kusambaa athari za majanga , watumisi wa umma walio msitari wa mbele wanahitaji kuwa tayari wakati wote katika mazingira ya kudhibiti na kuzuia na zaidi ya yote kufuatilia watu wanaoshukiwa kupata maambukizi na pia kutoa elimu kwa umma view kipaumbele vua harakati zao za kudhibiti maambukizi.

Bwana. Bande amesema “Kama kuna somo lolote tulilojifunza kutokana na COVID-19 ni kwamba katika wakati wa dharura ari na wajibu wa watumishi wa umma unasalia kuwa muhimu sana.

Haki mtandaoni, kutoka Hispania mshindi wa tuzo ya utumishi wa umma UNPSA 2020
Digital Justice, Spain, 2020 UNP
Haki mtandaoni, kutoka Hispania mshindi wa tuzo ya utumishi wa umma UNPSA 2020

Ni lazima kujikita kuchukua hatua

Sasa kuliko wakati mwingine wowote janga la COVID-19 limeonyesha umuhimu wa hatua madhubuti na zinazofanyakazikwa sekta ya umma ili kukabiliana na majanga.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt. Tedross Ghebreyesus katika maadhimisho hayo amesema “Sote tumetambua uwezo na mnepo wa watumishi wa umma hususan mamilioni ya wafanyakazi walio msitari wa mbele ambao wanahakikisha mifumo yetu inaendelea kufanyakazi “

Pamoja na kwamba amesema kuwa ni haki kuwapongeza na kuwasherehekea watumishi wa umma swali ni je “Sisi tunafanya nini kwa ajili ya watu hawa?”

Mkuu huyo wa WHO amesisitiza kwamba janga la corona linaendelea kuongezeka na idadi ya wagonjwa na vifo vinaongezeka hivyo “ Tuna kibarua kikubwa cha kufanya ikiwemo haja ya kuimarisha uwezo wa sekta ya huduma kwa umma , kuwalinda watumishi dhidi ya unyanyapaa na udhalilishwaji na kuwezesha mifumo na sera za kuwasaidia wahudumu wa afya ili waweze kufikisha huduma inayotakiwa kwa umma.”