Ulimwengu wa Kiarabu ni wakati wa kugeuza janga la COVID-19 kuwa fursa: Guterres
Ulimwengu wa Kiarabu ni wakati wa kugeuza janga la COVID-19 kuwa fursa: Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi.
Guterres kupitia taarifa ya kisera kuhusu janga la COVID-19 na jinsi ya kujikwamua vyema katika nchi za ulimwengu aloyoitoa hii leo amesema janga hilo limedhihirisha mapungufu na hali tete katika jamii na uchumi duniani kote na ulimwengu wa Kiarabu haukusalimika.
Amesema ingawa ukanda huo umebarikiwa na mchanganyiko wa mambo na uwezo mkubwa lakini bado nchi zote ziwe tajiri wa mafuta, za kipato cha wastani au zenye maendeleo duni zote zinakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na janga hili lililoibua athari zingine “Uchumi wa kanda hiyo umepata mapigo mengi, kuanzia virusi lakini pia kushuka kwa kasi kwa bei ya mafuta, mapato kutoka nje na utalii. Matarajio ya kiuchumi ni ya chini kushuhudiwa kwa miaka 50. Na uchumi wa kikanda utarajiwa kusinyaa kwa zaidi ya asilimia 5 huku katika baadhi ya nchi ukishuka kwa tarakimu mbili.”
Ameongeza kuwa na wakati mamilioni ya watu wakisukumwa chini kiuchumi, robo ya watu wote katika ulimwengu wa Kiarabu huenda wakaishi katika umasikini.
Katibu Mkuu amekumbusha kwamba ukanda ambao tayari umeghubikwa na mizozo na pengo la usawa hali hii itaongeza athari kubwa zaidi za kisiasa na utulivu wa kijamii.
Ametaja waathirika wakubwa kuwa ni wanawake na wahamiaji ambao wanawasilisha asilimia 40 ya nguvu kazi ya ukanda huo, ambao pia tayari una watu milioni 55 wanaotegemea msaada wa kibinadamu ili kuishi.
Pamoja na changamoto hizo Guterres amesema COVID-19 inaweza kuwa fursa kubwa kwa ulimwengu huo kutatua migogoro ya muda mrefu na kushughulikia changmoto za kimfumo na amependekeza vipaumbele vinne vitakavyowaongoza kujikwamua vyema na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ambavyo ni
Ukurasa kuhusu Virusi vya Corona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.“Mosi hatua za haraka za kupunguza kusambaa kwa maambukizi, kukomesha migogoro na kukidhi mahitaji ya harama ya walio hatarini, Pili kuongeza juhudi za kuzipa pengo la usawa, tatu kupiga jeki ukwamuaji wa kiuchumi na nne sasa ni wakati wa kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu.”
Amesisitiza kwamba kwa pamoja ukanda huo unaweza kubadili mgogoro huu kuwa fursa na kuleta faida kubwa sio tu kwa ukanda huo bali kwa dunia nzima.